Tuesday 28 September 2010

KWENU WADANGANYIKA

Hivi karibuni kwenye blogu mbali mbali, kumekuwa na mwelekeo hasi wa kukatisha tamaa watanzania wanaoamua kukaa nje ya nchi. Tanzania ina kiwango kidogo sana cha ‘diaspora’ kulinganisha na idadi yetu ya watu.

Wengi wetu ndio tumenza hivi karibuni ku ‘DARE’ kuweka makazi nje ya
nchi, wengi wetu ni ‘FIRST GENERATION.’ Nchi nyingine kama majirani
zetu na hasa ‘West Africa’, tayari wana ‘third au fourth generation
diaspora.’ Diaspora wao wamejiimarisha nje ya nchi na wanasaidia nchi
zao kwa njia moja au nyingine kwa mfano:

Moja, kutambulisha nchi zao huko waliko (Tanzania haijulikani sana,
moja wa sababu ni kwamba watu wa nje hawajakutana na watanzania!),
mbili, wanapeleka ndugu zao nje ya nchi, kwa masomo na kazi; tatu
wanawekeza kwenye nchi zao; na nne kwa mafanikio yao, wanaletea sifa
nchi zao za asili walikotokea, kupitia kushiriki kwenye michezo,
mafanikio kitaaluma, kikazi, kibiashara, nk.

Kwa upande wa mahusiano ya kindoa, Barrack Obama ni uzao wa aina hii.
Obama asingekuwepo kama si mjaluo kufanya mavituz huko Hawaii! Mfano
mwingine ni kama Adebayo Ogunlesi, yule Mnigeria aliyenunua ‘London
Gatwick Airport.’

Vile vile kuna wanamichezo, wanamuziki lukuki wa Ghana, Nigeria, etc
ambao ni ‘third generation dispora.’ Vile vile kuna ‘ first generation
diaspora’ wameingia kwenye jukwaa la siasa Ujerumani, Uingereza, nk.

Ghana ina idadi ndogo ya watu na haina vivutio vyovyote vya utalii
kulinganisha na sisi, lakini inajulikana zaidi ya Tanzania sababu ya
nguvu ya ‘diaspora.’ Mara nyingi nikisafiri watu wananiuliza kama nini
ni Mghana. Sijawahi kuulizwa kama mimi ni Mtanzania!

HATA KAMA MTU LEO ANABEBA BOKSI NJE YA NCHI, BADO KUNA UWEZEKANO MTOTO
WAKE, MJUKUU WAKE, AU MTUKUU WAKE AKAWA MTU WA MAANA HUKO NJE ALIKO.

Hao “third generation diaspora” wa nchi nyingine ambao wana mafanikio,
SI KWAMBA BABU au BIBI ZAO WALIKWENDA NJE WAKIWA MATAJIRI.

Wengi wao wali ‘struggle,’ na hata kama hawakufika mbali, kizazi chao
cha sasa wanaona faida. Mapambano ya kweli ya kimaisha, kimaendeleo na
kidunia hayako Dar es salaam , Bukoba, Mbeya au Lindi, etc, yako New
York, London, Los Angeles, Tokyo, Paris, etc.

Huko watu wanapambana na DUNIA. Mimi naona ATTITUDE YETU TULIYORITHI
KWENYE UJAMAA BADO INATU “HAUNT” NDIO MAANA TUNARIDHIKA NA KIDOGO
TUNACHOPATA TANZANIA, TUNAOGOPA USHINDANI NA KUKEJELI WANAOJARIBU
MAISHA NJE.

MTANZANIA AKISHAKUWA NA NYUMBA NA GARI ANAONA AMEFIKA! lakini mtu wa
“West Afrika” hata kama vitu hivyo anavyo, atafikiria njia nyingine za
kuji ‘establish’ zaidi nje ya nchi.

Na ndio maana mipango ya ‘East African community’ inapoendelea
watanzania wanaanza KUOGOPA na KUTETEMEKA! Ni kwa sababu hawajazoea
ushindani wa kidunia, wanaridhika tu na wanachopata nchini.

‘Utajiri wa Watanzania haufikii viwango vyovyote vya kimataifa! Sasa
hivi Tanzania kuna makampuni mengi ya Kenya, lakini hakuna makampuni
ya Tanzania Kenya!.

Watanzania tusiwe na mtazamo wa karibu (MYOPIC), tuone mbali.
Tusifikirie mafanikio yetu, bali ya vizazi vijavyo, wajukuu na watukuu
wetu. KAMA MTU YUKO NJE ANABEBA BOKSI HATAKI KURUDI, MWACHE SABABU
WATOTO, WAJUKUU AU WATUKUU ZAKE HUKO NJE WANAWEZA KUWA NA FAIDA KWA
NCHI YETU.

‘Afterall,’ uzoefu unaonesha hao ‘first generation diaspora,’ mbao
siku hizi tunaitwa wabeba boksi, umri ukiongezeka huwa tunarudi
Tanzania! Wanaozeekea nje hadi mwisho wa maisha yao mara nyingi ni
'generation' zinazofuata. Nadhani ujumbe umefika!

Na Leila Abdul - MwanaBIDII


asente,
na zaidi wakati wenzetu toka mataifa afrika wanapiga hatua na kusaidiana. sisi ndio kwaaanza tunajisifu kwa kumchomea mtu migration ili arudishwe kwao akale ndondo na dona.wakati wewe unafaidi vibawa,lamb na hons peke yako, mwisho unakuja kufa kwa cholesterol na ugonjwa wa moyo bure kwa roho mbaya.tuache roho mbaya wabantu kha.vibawa na hons vipo tu havitaisha,sio ukiona mwenzio kaja tafuta maisha unanuuuna utadhani memba wa sweden demokrat.wakati maganga wenzio wamejazana huko nyumbani maneromango, na hawaoni dili kubaki nyumbani kulijenga taifa.

No comments:

Post a Comment