ALI KIBA
Mwanamuziki wa Kizazi kipya Ali Kiba ambaye alikuwa aende nchini
Marekani kwa maonesho kadhaa nchini humo amegonga mwamba mara baada ya
ubalozi wa Marekani Kumnyima Viza ya kumruhusu kuingia nchini humo.
Chanzo chetu cha habari kinasema Mwanamuziki huyo Mahiri ambaye
anakubalika sana huko Ulaya na Marekani alifika Ubalozini hapo leo
asubuhi kwa ajili ya kushughulikia Viza yake ili aweze kwenda nchini
Marekani lakini aliambiwa na mmoja wa maafisa wa Ubalozi huo kuwa hawezi
kupata Viza kwa sababu ya matatizo ya Pasipoti yake ya kusafiria.
Hata hivyo inasadikika kwamba huenda mwanamuziki huyo alikuwa hajakagua
pasipoti yake ambayo inaelekea imaisha hivyo alitakiwa kuomba nyingine
kabla hajaenda kuomba Viza, lakini hakufanya hivyo! labda alikuwa hajui
kama Pasipoti yake imeisha au huenda alikaidi kufuata utaratibu huo
ambao umepelekea kumkwamisha katika safari yake hiyo.
Ali Kiba ametoka Ubalozini hapo akiwa mwenye kunyong'onyea na kukata
tamaa kwani haijajulikana kama angefanya onesho siku gani huko Marekani.N:B.jamaa washaanza kubana maana hawatupendi kweli.
No comments:
Post a Comment