TAARIFA
YA LADY JAYDEE KWA VYOMBO VYA HABARI , KUHUSIANA NA UBALOZI WA WANAWAKE
WENYE UGONJWA WA FISTULA KWA KUSHIRIKIANA NA HOSPITALI YA CCBRT
HABARINI ZA ASUBUHI NA ASANTENI SANA KWA VYOMBO VYA HABARI KUITIKIA WITO HUU
KAMA MWANAMUZIKI WA TANZANIA, NASHUKURU KUWA JAMII YA WATANZANIA WENZANGU WANAPOKEA VIZURI KAZI YANGU YA SANAA YA MUZIKI.
KWA
JINSI HIYO BASI……, NA MIMI NINALO JUKUMU LA KURUDI KWA JAMII YANGU NA
KUSHIRIKIANA NAO KATIKA HARAKATI ZA KUJIKWAMUA KUTOKA KATIKA MATATIZO
MBALIMBALI KAMA VILE MAGONJWA NA UMASIKINI.
NINAYO FURAHA KUWAFAHAMISHA KUWA, MIMI KAMA MSANII NINAE ANGALIWA NA KUSIKILIZWA NA JAMII YA WATU WENGI PANDE MBALI MBALI ZA TANZANIA.
LEO HII NIMEUNGANA NA HOSPITALI YA CCBRT KUWA SHUJAA WA WANAWAKE WANAOSUMBULIWA NA FISTULA.
UAMUZI HUU UMEKUJA BAADA YA CCBRT KUNIALIKA KUTEMBELEA WODI MBALIMBALI ZA WAGONJWA ZILIZOPO HOPITALINI HAPA.
LAKINI
BINAFSI NILIGUSWA ZAIDI NA WANAWAKE WANAOSUMBULIWA NA UGONJWA WA
FISTULA, UKIZINGATIA PIA MIMI NI MWANAMKE NIKAKUBALI KUUNGANA NA CCBRT
ILI KUSAIDIA KWA HALI NA MALI KUOKOA MAISHA YA WANAWAKE WALIO WENGI..
TANGU
NIZALIWE MPAKA NAKUWA MKUBWA NA KUFIKIA HATUA NILIOPO HIVI SASA, NAKIRI
SIKUWAHI KUSIKIA WALA KUONA MGONJWA WA FISTULA. MPAKA NILIPOTEMBELEA
HOSPITALI YA CCBRT
NIMESIKITISHWA
ZAIDI BAADA YA KUELEZWA KUWA WANAWAKE WENGI WENYE UGONJWA HUU HUSHINDWA
KUFANYA KAZI WAKATI MWINGINE HATA KUTENGWA AU KUJITENGA NA JAMII ZAO
WANAMOISHI KUTOKANA NA KUWA WANAVUJA HAJA NDOGO AU HAJA KUBWA KILA MARA
BILA WAO WENYEWE KUPENDA WALA KUJIJUA. KWAKUWA WANAKUWA WANASHINDWA
KUJIZUIA.
HIVYO KUPELEKEA WANAWAKE HAO WENYE FISTULA KUENDELEA KUISHI MAISHA DUNI YA UPWEKE NA KUENDELEA KUWA MASKINI
LABDA NIONGELEE KWA KIFUPI KUHUSIANA NA FISTULA.
NI
UGONJWA UNAOWAPATA WASICHANA NA WANAWAKE WAKATI WA KUJIFUNGUA NA HII
HUTOKANA NA KUSHINDWA KUFIKA VITUO VYA AFYA VYENYE HUDUMA YA UZAZI.
FISTULA NI UGONJWA UNAOZUILIKA NA UNATIBIKA.
HAKUNA
MWANAMKE ANAETAKIWA KUISHI NA FISTULA HASA UKIZINGATIA CCBRT INATOA
MATIBABU, USAIFIRI, CHAKULA NA MALAZI BURE KWA WAGONJWA WOTE
WANAOSUMBULIWA NA FISTULA.
JUKUMU
LANGU KUBWA KATIKA UBALOZI HUU NI KUSIMAMA NA KUTUMIA SAUTI YANGU, NA
NAFASI NILIONAYO KATIKA JAMII KAMA MWANAMUZIKI KUTOA WITO KWA WAGONJWA
WENYE FISTULA NA HATA WALE WANAJAMII WENGINE WOTE WANAOFAHAMU WAGONJWA
HAO, WAJE CCBRT KUPATA MATIBABU NA HUDUMA ZOTE BURE.
NITAFANYA
HAYO POPOTE NITAKAPOPATA NAFASI YA KUONGEA NA JAMII INAYONIZUNGUKA, AMA
IWE KATIKA MAONYESHO YANGU AU MAHOJIANO NA VYOMBO VYA HABARI.
NITAFANYA
HIVYO PIA KATIKA MITANDAO YA KIJAMIII, NINAYOHUSIKA NAYO KAMA BLOGS NA
FACEBOOK NA HATA KATIKA MATANGAZO YA TV, RADIO NA VIPEPERUSHI.
ILIMRADI TU UJUMBE UWAFIKIE WANAWAKE WENYE FISTULA WAJE KUTIBIWA BURE CCBRT.
NDUGU ZANGU WAANDISHI WA HABARI, NAOMBA MJIUNGE NAMI KUWA SHUJAA WA WANAWAKE WENYE FISTULA
ASANTENI SANA
No comments:
Post a Comment