hapa ni jirani na eneo ambalo ilikuwa ofisi ya mzee kipindi hicho
(jengo hilo nyuma kulia lenye bati nyekundu)
hii barabara kushoto hapo mbele (sombrero hotel) ndio mzee alipata ajali
na hii ndio hotel yenyewe palee kwenye rangi ya orange iliitwa sombrero,ndio hapo mzee alitoka kisha kuanza kupandisha kuelekea huku inakoelekea suzuki na akapata ajali hapo mbele kidoogo.
ILIKUWA NI SIKU KAMA YA LEO TAR 16-2-1988 MIAKA 23 ILIYOPITA,NILIMPOTEZA BABA YANGU MZAZI KWA AJALI YA PIKIPIKI
NI PALE AMBAPO KAMA UTANI RAFIKI YAKE ALIPOKUJA KUTUGONGEA USIKU WA MANANE NA KUTUPA TAARIFA KWAMBA MAREHEMU MZEE AMEPATA AJALI NA YUKO MZIMA(TULIDANGANYWA)ILA ANA HALI MBAYA (KUMBE KAFA ON THE SPOT)
NI TUKIO AMBALO LILITOKEA GHAFLA SAANA KIASI AMBACHO MPAKA LEO HII HUWA NAFIKIRIA KAMA VILE YUPO TU KAJIFICHA MAHALI IKO SIKU ATAJITOKEZA.
LAKINI UKWELI NDIO HUO KWAMBA ALIFARIKI TOKA SIKU HIYO NA HATUJAWAHI KUMUONA TENA ZAIDI YA KUMCHUNGULIA MARA YA MWISHO ALIPOKUWA ANAZIKWA,
NI TUKIO AMBALO HUWA SIPENDI KULIKUMBUKA KATIKA MAISHA YANGU MAANA BAADA YA HAPO NDIO KIPINDI AMBACHO MIMI NA FAMILIA YANGU YOTE TULIPOANZA KUONJA LADHA NA MACHUNGU YA DUNIA HII.
KATIKA KIPINDI CHOTE HIKI CHA MIAKA (23)TUMEWEZA KUJIFUNZA ELIMU DUNIA VIZURI SANA NA IKATUINGIA AKILINI KIASI AMBACHO KAMA INGEKUWA INATOLEWA SHAHADA TUNGEPATA PHD YA ELIMU DUNIA.
LAKINI YOTE TUNAMSHUKURU MUNGU MAANA TUMEWEZA KUVUKA VIZINGITI VYOTE NA MAJARIBU YA KILA NAMNA.NA MPAKA LEO BADO TUNAPATA MAJARIBU LAKINI TUNAENDELEA NA TUTAENDELEA KUSIMAMIA KIDETE KWAMBA TUNAYASHINDA.
MDAU HABARI YA KUONDOKEWA NA MZAZI WAKATI BADO U MDOGO TEGEMEZI ISIKIE HIVYO HIVYO,USIOMBE YAKUKUTE HATA SIKU MOJA,NASHUKURU MUNGU NIMEYAPITIA YOTE HAYO NA MPAKA LEO NIMEWEZA KUSIMAMA MWENYEWE KWA NGUVU ZA MWENYEZI MUNGU.
MWISHO PIA NAMSHUKURU MUNGU KWAMBA KATIKA TAREHE HIZIHIZI MWEZI HUU NATEGEMA KUPATA KIJANA (NASAR JR) NAMWOMBA MUNGU AMSAIDIE MKE WANGU AJIFUNGUE SALAMA AMINA.
MUNGU AENDELEE KUMLAZA PEMA PEPONI KWA AMANI BABA YANGU MPENDWA
R . I . P .
NAZARETH ANYELWISYE MWAMGOGWA
AMINA
hii habari inasikitisha sana.Pole sana kwakuondokewa na mzazi wako,ndio hali ya dunia hauko peke yako wengi wanapoteza wazazi wangali wakiwategemea. Hii ni mipango ya mungu inabidi tushukuru kwa kila jambo kwani kazi ya mungu haina makosa.nyie mlimpenda baba yenu lakini mungu alimpenda zaidi.mshukuru mungu kwakukuwezesha kufika hapo ulipo bila ya baba bali ukumbuke ya kwamba yeye aliye juu ni baba wa yatima ni bwana wa wajane.endelea kumwamini kwani yeye atakufariji kwa njia pekee na wala hutapungukiwa atajaza palipopungua na atakufuni usipitiwe na baridi.
ReplyDeleteNASHUKURU SANA MDAU KWA MANENO YAKO YA MATUMAINI,UBARIKIWE SANA
ReplyDelete