Thursday 17 March 2011

lunch time leo"UGALI MAINI MCHUZI + MCHICHA


maini,nyanya na vitunguu vikiwa tayari

kaaanga nyanya na vitunguu kama kawaida mpaka viive,kisha weka cury powder na maini,changanya pamoja na nyanya huku ukigeuza geuza kama dk 5.weka garlic na pilipili(option)

kisha weka maji kikombe kimoja na beef cube 1 changanya pamoja

baada ya dk 5 zingine sauce ya maini itakuwa tayari kwa kuliwa

"voilaaa"
hapa ndio mwisho,waweza kula kwa kitonge ama wali na mchicha ulikuwa tayari umekaangwa na mafuta na kitunguu tu.enjoy

INGREDIENTS
*500 gm maini au figo au mix
*nyanya zilizokatwa au za kopo
*kitunguu kimoja
*curry powder kijiko kimoja
*chumvi kiasi chako
*kitunguu saumu kilichosagwa kijiko 1
*beef builoin  cube1pc.

wadau mara nyingi recipe yangu huwa inakuwa simple ni kwa ajili ya matumizi ya nyumbani,na ndio maana siweki vitu complicated.nafanya hivi ili kila mtu anayetaka kupika iwe rahisi kupata hayo mahitaji.najua nikiweka recipe za ki hotelia zaidi nitawakwaza na nia ni kuelekezana tu namna ya kupika mwenyewe chakula kizuri unapohitaji.

3 comments:

  1. Chakula kina mvuto mpaka njaa inauma sasa!hongera @kaka Isaac kwa kupenda kupika, kwani unapata kitu bora na roho inapenda!!!!!

    ReplyDelete
  2. ha ha haa,kula kwa picha km wapare dada.tengeneza nyumbani maini kibao huko.

    ReplyDelete
  3. hapa naona nimechelewa sijui nilikuwa wapi...yaani mate yananvyonidondoka ....

    ReplyDelete