Tuesday 10 May 2011
Mabanda 73 ya Wabara yateketezwa Zanzibar
MABANDA 73 ya wafanyabiashara wa Tanzania bara katika fukwe za Mchangani na Kiwengwa, katika Mkoa wa Kaskazini Unguja, yameteketezwa kwa moto.Mabanda hayo ya maduka yaliyokuwa yakilimikiwa na wafanyabiashara 40 yalichomwa moto usiku wa kuamikia juzi.
Habari zilisema mabanda 43 yalichomwa katika ufukwe wa Mchangani, katibu na Hoteli ya Waikikina mengi 30 yaliteketezwa katika ufukwe wa Kiwengwa karibu na Ocean Beach Resort.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kaskaskazini Unguja, Masoud Msellem Mtulya, aliwaambia waandishi wa habari jana polisi wanawashikilia watu saba, wakihusishwa na matukio hayo.
Mtuya alisema watu hao watafikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa.Alisema polisi pia wanaendelea na msako dhidi ya watu wengine wanaohusika na tukio hilo na aliwaomba wananchi, kutoa ushirikiano utakaowezesha kukamatwa kwa watu hao.
Akizungumzia chanzo cha matukio hayo, Kamanda Mtulya alisema ni madai ya wananchi wa maeneo hayo kuwa wafanyabiashara hao wa vinyago na mama ntilie, wanajihusisha na vitendo vya kuuza na kuvuta bangi na ukabaha kwa wanawake.
Alisema wananchi hao, wanadai kuwa mambo hayo yamekuwa yakifanyika hadharani, ndani ya maeneo ya fukwe hizo.Kwa mujibu wa kamanda, wananchi hao pia wanadai kuwa wanafanyabiashara hao wanaendesha shughuli zao bila vibali.
Hata hivyo watu ambao mabanda yao yameteketezwa, walisema kitendo hicho cha ukatili kimefanywa kwa sababu ya kuwachukia watu wa Tanzania bara.
Walisema wananchi wa maeneo hayo hawapendi kuwaona watu wa Tanzania bara wakijihusisha na biashara za kitalii.
Hata hivyo Kamanda Mtulya alisema madai ya wananchi wa maeneo hayo hayana msingi hasa ikizingatiwa kuwa vitendo vya uhalifu, havifanyiki katika Mkoa wa Kaskazini Unguja pekee.
"Lakini pia suala la watu wa Tanzania bara kufukuzwa, halina ukweli kwa sababu wengine ambao mabanda yao yameteketezwa ni Wazanzibari ingawa watu wa Tanzania bara ni wengi," alisema.
Kamanda Mtulya alisema hata hivyo, polisi wanalichukulia tukio hilo kuwa ni la uhalifu na kwa hiyo haliwezi kumalizwa kienyeji.Alisema kwa msingi huo, polisi watakawasaka wale wote waliohusika katika tukio hilo ili wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria.Wakati huo huo, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, imeviagiza vyombo vya usalama kushughulikia ipasavyo suala hilo.
Agizo hilo lilitolewa jana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi baada ya kutembelea maeneo hayo na kushuhudia uharibifu mkubwa wa mai.
Balozi Idd ambaye aliwapa pole wafanyabiashara hao, alisema serikali imesikitishwa mno na tukio hilo na kwamba itachukua hatua za kuhakikisha vitendo vya aina hiyo, vinakoma.
Hata hivyo Makamu wa Pilisi wa Rais, aliwataka wamiliki wa mabanda yaliyoteketezwa, wasilihusishe tukio hilo dhidi ya watu wa Tanzania Bara.Alisema watu wote waliowaathiriwa na ukatili huo wanapaswa kujiona kuwa wote ni Watanzania wenye haki ya kufanya biashara katika eneo lolote la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama inavyoelekeza na katiba na sheria za nchi.
Kuhusiana na ombi la wananchi hao kutaka kupatiwa hifadhi ya muda, Balozi Seif Serikali ya Mkoa itawapatia sehemu ya kulala kwa muda wakati serikali ikilishughulikia suala hilo.
Waathirika wa tukio hilo waliiomba serikali kuchukuwa hatua zinazofaa dhidi ya waliohusika.Akizungumza kwa niaba ya wenzake, James Charles Chacha alimshukuru Balozi Idd kwa kuwafaraji walioathiriwa na tukio hilo.
Pia alielezea kuridhishwa kwake na hatua zinazochukuliwa na serikali kukomesha kadhia hiyo.Charles Pendael Tito, alisema kwa sasa wanaishi kwa hofu inayotokana na uwezekano wa waliohusika, kuendeleza vitendo hivyo na kuiomba serikali imarishe ulinzi.
Tukio hilo, limekuja miezi kadhaa baa ya watu wasiojulikana, kuendesha opereshe ya kuchoma moto majengo ya biashara za baa, yanayomilikiwa na watu wa Tanzania bara.
mwananchi
wazanzibari wabaguzi sana ,shule inamuhimu jamani mwenye upeo hana ujinga kama huo
ReplyDelete