Friday 3 June 2011

lunch time leo"NDIZI & NYAMA/BANANA STEW"enjoy

kwanza unatakiwa kuwa na ndizi

kisha nyama ya mfupa hasa mbavu

ukishakata nyama vipande chemsha na tangawizi na kitunguu swaumu
ndizi zilizo tayarishwa tayari

katakata kitunguu,carrot,hoho au cerel

kazi na dawa

kaaanga vitunguu nyanya na hizo mboga zingine kwenye mafuta mpaka ziive
zikiiva utaweka nazi ya kutosha na maziwa mgando(yoghurt)
kisha unakoroga zichanganyike

baada ya hapo utaweka ndizi zilizomenywa kwanza kisha juu utaweka nyama iliyokwisha chemshwa tayari 

kisha ile supu yoote ya nyama unamwagia juu ya hizo ndizi nyama

itakua hivi baada ya kuweka supu,then unafunika na kuiacha zichemke pamoja dk 15 au 20

hapa mzigo uko tayari kwa kuliwa


enjoy draft hiyo
MAHITAJI
*ndizi za kutosha
*nyama ya mfupa 1kg
*kitunguu 1
*hoho1
*carrot 2
*nazi kopo 1 kubwa au mbili ndg
*yoghourt 1
*kitunguu swaumu na tangawizi
*chumvi kiasi

3 comments:

  1. Ahsante kwa mlo mtamu nimeupenda ngoja nifanya msako wa ndizi nami niandae:-)

    ReplyDelete
  2. Jamani kakangu kumbe uko makini hivi kwa upande huu...chakula kinanivuta mie. Itabidi leo nizitafute ndizi kwakweli..

    ReplyDelete
  3. chakula kizuri sana kinatamanisha kweli asante kwakutuonyesha mapishi likini hii ni mtazamo wangu samahani kama nitakukwaza na hili mbona sufuria inaonekana kama nyeusi sana utafikiri ni kama zile za kwetu zinazotumiia moto wa kuni?

    ReplyDelete