KWA WALE WENZETU HAWAPENDI HII KITU LEO MTATUPISHA KIDOGO
Unatakiwa kuwa na vipande vya pork ribs vilivyokatwa kama hivi
baada ya marination"garlic+ginger paste,salt and lemon"inakua hivi then unaiacha ndani ya friji(km una muda) saa nzima ili viungo vikubali
baada ya hapo unatumbukiza ndani ya karai yenye mafuta moto yaliyochemka unaziacha humo huku ukigeuza geuza mpaka ziwe brown
pembeni tengeneza kachumbari yako km hivi,usisahau piri piri
naam baada ya kuwa tayari mkuu wa meza ataonekana kama hivi
na hapo draft imekamilika,kitonge na hiyo kitu ndio haswa nyumbani kwake
ANGALIZO
kuna wadau wawili watatu walikua wanauliza "mzee isaackin unamaliza kitonge chote hicho?,hapana kabisa,huwa napika ugali mkubwa lakini sijawahi kumaliza mara nyingi napiga nusu na nusu ingine kesho au mchana na usiku,kula ugali mkubwa namna hii ni hatari kwa afya yako ingawa ni janga la kitaifa.
pia asanteni kwa kuijali afya yangu
msisahau baada ya kujinoma hii kitumoto partner wake ni hilo kopo unaliona hapo
baada ya hapo lazima upige usingizi wa pono
MAHITAJI
*thick pork ribs 1kg
*ginger&garlic paste 2 tbspoon
*fresh lemon juice 1
*salt to taste
NAMNA YA KUPIKA NI KAMA NILIVYOWEKA CHINI YA PICHA
NDUGU WADAU,SAMAHANI SANA KWA KUTOWEKA RECIPE KWA MUDA MREFU,NAJUA WENGI WENU MNAPENDA SANA HII SEHEMU,ANYWAY BAADA YA KUKAA NIKAFIKIRIA KUTENGENEZA KITIMOTO KAMA CHA NYUMBANI,NDIO MAANA UTAONA SPICE ZAKE ZILIKUWA SIMPLE KABISA.UKWELI ILITOKA VIZURI NA TASTE YAKE ILIKUA TAMU KUPITILIZA"I WISH MNGEKUWEPO"
HATA HIVYO ILE YA HOME KINO PALE KWA MZEE RINGO,AU SINZA B.B,AU M"NYAMALA GARAGE KWA PROSPER AMA A KWA BABU PALE NYUMA ILE KIBOKO,SIJUI HUWA WANATUMIA NINI WALE.
BY THE WAY KIUBISHI HATA HII ILITOKA MUKIDE KIMTINDO
KAA TAYARI KWA RECIPE ZINGINE
asante kaka isaackin recipe ya kitimoto japo umeadimika kwa mudakaka mimi nilikuwa naomba unisaidie recipe ya chapati kama unajua jinsi ya kutengeneza mimi huwa napenda sana chapati lakini nikipika hazitoki laini zinatoka ngumu naomba kama unajua namna yakuziandaa zizitoke ngumu pls nieleweshe kupitia hii glob yako mimi ni fan wako mkubwa ubarikiwe na kazi yako nzuri nasubiri majibu kwa hamu
ReplyDeleteanakusalimia AZIZ TAYLOR
ReplyDelete