Asasi ya utafiti wa vyakula salama
Tanzania (TAHEFORO) inatarajia kutoa tuzo ya upishi bora Tanzania (Bema Chef’s
Award Tanzania) kwa lengo la kuendeleza ubunifu wa sanaa ya mapishi ya vyakula
vya asili ya Kitanzania.
Hayo yamesemwa leo
jijini Dar es Salaam na mwenyekiti wa asasi hiyo Bw. Benedict Maato wakati
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu azma ya asasi yake kuanzisha tuzo
hiyo.
Amesema kuwa tuzo hiyo itakuwa
ikisimamia ubunifu na uendelezaji wa sanaa ya mapishi ya vyakula vya asili
ambavyo vipo katika hatari ya kutoweka.
“Jamii yetu leo, tumeacha kula
vyakula vyetu vya asili ambavyo vina virutubisho vingi vya asili na usalama kwa
afya zetu, badala yake tunapendelea kula vyakula hivi vya kisasa ambavyo vina
matatizo makubwa kwa afya zetu” amesema Bw. Maato.
Amefafanua kuwa tuzo hiyo itakuwa
ikishindaniwa kila mwaka ili kupata Wapishi bora wa vyakula vya
Kitanzania, Mgahawa bora unaotoa huduma ya vyakula vya asili, vituo bora vya
Redio na Luninga viinavyorusha vipindi vya mapishi ya
vyakula vya asili, Waandishi bora wa makala au vitabu vya mapishi ya vyakula
vya asili na Watafiti bora wa vyakula vya
asili.
Aidha
mwenyekiti huyo amebainisha kuwa lengo kubwa la utoaji wa tuzo hiyo ni kurudisha
sanaa ya mapishi nchini na kusisitiza kuwa
washiriki wote watakaoshindania tuzo hiyo watatakiwa kuonyesha ubunifu wao katika kupika vyakula
hivyo na kutoa wito kwa wananchi kupenda
kutumia vyakula vya asili
No comments:
Post a Comment