Friday 16 December 2011

ATHUMANI MACHUPA ATIMULIWA SWEDEN





SAKATA la wachezaji wa Kitanzania kuingia katika migogoro na klabu za Ulaya, limeendelea kuchukua sura mpya baada ya mshambuliaji, Athumani Machuppa, kutimuliwa na klabu yake ya Vasalund IF.
Habari za uhakika zimeeleza, uongozi wa Vasalund IF umeamua kuachana na Machuppa baada ya kuchoshwa na vituko vyake.
“Kila akienda kuichezea timu ya taifa, alikuwa anachelewa sana kurudi. Mara ya mwisho hakurudi kabisa na kuna taarifa alikuwa anatafuta timu Tanzania,” kilieleza chanzo.
Vasalund IF imeamua kuvunja mkataba na mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba huku ukiwa umebakiza si zaidi ya miezi mitatu.

Machuppa alikuwa mmoja wa wachezaji tegemeo wa Vasalund IF, lakini inaonekana vituko vimeifanya klabu hiyo kunyoosha mikono na kumuacha. Taarifa zinaeleza, Machuppa amekuwa akionekana katika mitaa ya Jiji la Dar es Salaam.
Kwa upande wa Sweden, ligi daraja la kwanza imefikia tamati huku Machuppa akishindwa kucheza mechi tano za mwisho kwa kuwa hakurejea katika kikosi chake kwa wakati mwafaka.
Mtanzania mwingine aliyewahi kuingia kwenye mgogoro na klabu yake ni Haruna Moshi ‘Boban’ aliyekuwa akiichezea Gefle IF ambayo pia ni ya Sweden.

chanzo:champion

2 comments:

  1. FOR FUCK SAKE LEAVE MY BABY ALONE YOU GUYS DON'T YOU HAVE BETTER THINGS TO TALK ABOUT??????????

    ReplyDelete
  2. hahahahahahahahahahahha utatukana vyombo vingapi vya habari!!!teh teh teh!!!!!kaaaaaazi kweli kweli!

    ReplyDelete