spika wa bunge mama anne makinda
ikiwa ni juzi tu hapa katibu wa bunge kakanusha kuhusu ongezeko la posho,katika hali ya kushangaza kama sio kusikitisha jana spika wa bunge mama makinda amethibitisha wabunge kuongezwa posho(sitting allowance) hadi kufikia sh 200,000.
spika makinda amedai wabunge wameongezewa posho hiyo kwa madai kwamba maisha kwa sasa dodoma yamekuwa ghali sana hasa nyumba za wageni wabunge wanazofikia bila laki moja hupati!
labda mama anna anafikiri watu hatuijui dodoma ama hatujawahi kufika.dodoma gesti na lodge zinaanzia kwa bei ya chini kabisa 3000 na kuendelea mpaka kufika huko kwa laki moja kama ukitaka.
madai mengine ya kusema kwamba maisha yamepanda dodoma yanazidi kutia machungu kwa wananchi kwani spika hajui kwamba maisha siku hizi ni aghali si dodoma tu bali tanzania nzima?na je kwa wafanyakazi wa kawaida hapo dodoma na kwingineko mbona hawaongezwi mishahara kwa sababu ya maisha ni magumu?
wanafunzi kila siku wanapigwa virungu na mabomu wakiandamana ili waongezwe chochote
inawezekana vipi mbunge alipwe posho 200,000+per diem80,000+50,000za mafuta=330,000/= per day nje ya mshahara wakati mfanyakazi wa kima cha chini analipwa pesa haifiki hata 200,000 kwa mwezi?
inasikitisha kuona kwamba wabunge tuliowachagua ndio wanaokuwa mstari wa mbele katika kufuja chochote kilichobaki katika nchi hii.
kichekesho ni pale spika mwisho wa taarifa hiyo alipotoa macho na kusisitiza kwamba tutakua wakali kuhakikisha wabunge hawachukui hiyo pesa mpaka wasign asubuhi na jioni ndipo tuwalipe,
kwani kuna asiyejua kwamba wabunge wengi wana sign na kuondoka kwenda kwenye mishe mishe zao huku wengine wakisign na kuingia bungeni wanaishia kulala usingizi wa pono.
je hii nchi inaenda wapi jamani?viongozi wanajua hili jahazi linakoelekea?maana ni kama vile tunaendaenda tu hata hatueleweki tunaaelekea wapi.
habari zaidi bofya HAPA
No comments:
Post a Comment