lunch time leo"PILAU LA KUKU WA KIENYEJI"
kuku mzima wa
kienyeji"ama höns"akiwa tayari kasafishwa na kukatwakatwa
unanza kwa kutia huyo kuku ndani ya sufuria
unakaanga kwa kuchanganya na garlic, ginger,garam
masala mpaka anaanza kuwa brown,
hakikisha asikauke sana.kisha unaweka maji ya
kutosha.
halafu unafunika achemke mpaka alainike,muda 1 hr
ama zaidi huku ukiongeza maji.
baada ya kuku kuiva
na kulainika,unaipua na kuweka pembeni.
kisha unaweka sufuria
ingine motoni,weka mafuta kiasi,kitunguu,viazi ulaya,
unakaanga kwa pamoja
mpaka vitunguu vinaanza kuwa brown
,kisha unaweka garlic
paste,hiliki nzima kiasi,cinnamon nzima kiasi na cummin seed kiasi.
unakaanga huo
mchanganyiko mpaka vitunguu vinakuwa brown kabisa lakini visiungue
.kisha unaweka
vipande vya kuku na pilau masala kiasi kidogo tu maana viungo vingi ulivyotumia
vimo katika pilau masala.
unakaanga
pamoja.kisha unaweka mchele na ile supu ya kuku iliyobaki,
kisha unaweka chumvi
unakoroga pamoja vyoote mpaka vichanganyike,unafunika nakusubiri vichemke pamoja
kwa dk km 10,
kisha unapunguza moto
unaweka chini kabisa no 1,mlio sweden mnaelewa lakini kama unatumia jiko la
makaa pia bongo unaelewa namaanisha nini.
unaacha katika moto
huo mdogo kwa dk 45 ama saa nzima,mda huo kama una kabia ama kawine shushia
kabisa,au hata ukitaka kwenda cheza draft poa,ama hata ukitaka kwenda
ku-over-haul tumbo liwe tupu pia wewe tu.
baada ya muda huo
pilau lako sasa liko ready kwa kuliwa,usisahau kutengeneza kachumbari yako
mapema,recipe kachumbari wengi mnaijua au ni nyanya,kitunguu ndimu piripiri
unakata slice slice vyembamba kisha unachanganya na ndimu na chumvi.
pilau lako likiwa
tayari kusulubiwa na kachumbari kwa pembeni
hapa unatafuta mkeka
au kapeti unakaa,maana si stahili kulia mezani na umma wala kijiko hutapata
utamu wake
bila kusahau kilaji
baada ya msosi na si kabla,enjoy
baada ya kukosa
mwaliko nimeona nijumuike na wadau wangu idd hii pilau tunalilia hapa hapa
bloguni.karibuni
MAHITAJI
*kuku
mzima
*mchele
1/2 kg
*olive
oil 1 spoon
*garam
masala 1tea spoon
*garlic
paste 1 spoon
*ginger
paste 1 tea spoon
*cinammon
whole 1
*cummin
seed 1 tea spoon
*hiliki
nzima 1 tea spoon
MAHITAJI KACHUMBARI
*nyanya 2
*kitunguu
kikubwa chekundu 1
*ndimu
1
*pilipili
(ukipenda)1
Ahsante kaka na nawatakieni mlo mwema ila hapo naona kama inakosekana SAFARI ...LOL
ReplyDeleteha ha haa,da yasinta tuko pamoja,safari imekosekana ila duh nimeijaribu hiyo mi imenishinda kabsaa.naamka mgonjwa siku nikinywa
ReplyDeleteMmmmhh? pole sana basi siku nyingine jaribu KILI au Serengeti...
ReplyDelete