HISTORIA FUPI YA MAREHEMU FRANCO LUAMBO LUANZO MAKIADI
François
Luambo Luanzo Makiadi alizaliwa 6 July 1938, katika kijiji cha Soni
Bata magharibi mwa jimbo la Bas Zaire huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo. Wakati bado mchanga wazazi wake walihamia jiji la Leopodville
ambalo sasa linaitwa Kinshasa. Baba yake aliitwa Joseph Emongo alikuwa
mfanyakazi wa shirika la reli wakati huo mama yake alikuwa akiuza
maandazi sokoni. Alipofikia umri wa miaka saba alitengeza gitaa lake
akawa analipiga kwenye genge la mama yake ili kuita wateja.. Mwanamuziki
maarufu Paul Ebengo Dewayon ndie aliyegundua kipaji cha mtoto huyu na
kuanza kumfundisha rasmi namna ya kupiga gitaa. Mwaka 1950 akiwa na umri
mdogo wa miaka 12 alichukuliwa rasmi kama mwanamuziki wa bendi ya Watam
iliyokuwa inaongozwa na Dewayon. Kipaji chake kiliwashangaza wengi hasa
kwa vile alikuwa akionekana umbo lake kubwa kama gitaa analolipiga
lakini akiwa analipiga kwa umakini mkubwa. Akiwa na miaka 15 alirekodi
nyimbo yake ya kwanza Bolingo na ngai na Beatrice (Mapenzi yangu kwa
Beatrice). Wimbo huu aliutunga alipojiunga na bendi iliyokuwa
inamilikiwa na Studio za Loningisa. Kiongozi wa bendi hiyo Henri Bowane
ndie aliyeanza kufupisha jina la mwanamuziki huyu na kumuita Franco,
jina alilokuja kujulikana nalo maisha yake yote. Mwaka 1955 alianzisha
bendi akishirikiana na Jean Serge Essous bendi ilizinduliwa katika
ukumbi wa OK Bar, hatimae bendi ilichukua jina la OK Jazz kwa heshima ya
bar ambapo ilizinduliwa.Katika muda mfupi ikiwa na mwimbaji Vicky
Longomba(Baba yake Lovy Longomba) walianza kuwa bendi pinzani ya bendi
kongwe ya African Jazz iliyokuwa inaongozwa na Grand Kalle. Mwaka 1958
Essous na Franco kuwa kiongozi na mtunzi mkuu wa kikundi alichokuja
kukijenga kwa kuanzia watu 6 hadi kufikia watu 30 kwenye mwaka 1980.
Franco mwenyewe alikuwa anasema OK Jazz iliweza kutoa album 150 katika
miaka 30 ya bendi hiyo.Mwaka 1958 Franco alifungwa kwa mara ya kwanza
kwa kosa la uendeshaji mbaya wa gari siku ya kutoka kwake jela ilikuwa
kama shujaa katoka vitani. 1960 Vicky Longomba aliacha bendi. Lakini
wakati huo Kongo ilikuwa kwenye vuguvugu za kutafuta uhuru na nchi
ilikuwa si shwari Franco akahamia Ubelgiji. Baada ya Mobutu Sese Seko
kushika nchi na kukawa na amani katika nchi iliyoitwa sasa Zaire franco
alirudi 1966. Akashiriki katika Tamasha la Sanaa Za Afrika
lililofanyika Kinshasa 1966 na Franco akawa kipenzi cha serikali ya
Mobutu.
Franco
hakuwa tu mwanamuziki mzuri bali pia aliendesha vizuri sana biashara
zake za kurekodi na kampuni alizozianzisha wakati huo. Alikuwa na lebo
kama (Surboum OK Jazz, Epanza
Makita, Boma Bango and Éditions Populaires). Katika miaka ya 70 muziki
wa Kongo ulishika kasi sana Afrika na Franco akiongoza jahazi kwa nyimbo
kama Infidelité Mado, na akaendeleza kupiga mitindo mbalimbali
kama Bolelo na muziki uliotokana na ngoma za asili toka Kongo
zikichanganywa na mapigo kutoka Cuba na kuanza upigaji wa gitaa uliokuja
itwa Sebene.
Mwaka
1970 Franco alimpoteza mdogo wake ambaye nae alikuwa mpiga gitaa
mashuhuri Bavon Marie-Marie Siongo ambaye alifariki katika ajali ya gari
baada ya kuwa akiendesha gari kwa hasira baada ya ugomvi na kaka yake
wakigombea msichana ambaye nae alipata kilema kutokana na ajali hiyo.
Lilikuwa pigo kubwa kwa Franco kwa miezi kadhaa aliaacha hata kupiga
muziki. Baada ya hapo OK Jazz ilibadili jina na sasa kuitwa TP OK Jazz
na mwaka 1973 kutoa kibao kingine kilichotikisa Afrika ,AZDA. Wimbo
huu kwanza ulirekodiwa kama tangazo kwa ajili ya kampuni ya Volkswagen
VW. Mahusiano yake na Mobutu yalikuwa na mawimbi mara wakipatana mara
wakikosana kutokana na Franco kuwa anatumia nyimbo zake kukosoa serikali
ya Mobutu. 1970 Franco alikuwa ni Rais wa wanamuziki wa Kongo na pia
kuajiliwa na kampuni ya kugawa mirabaha ya wanamuziki. Aliendelea
kutajirika kwa kuweza hata kunua ardhi nchini Ufaransa, Ubergiji na
Kongo, na kuwa na nightclub 4 kubwa kuliko zote Kinshasa kwa wakati huo
na kufanya club ya
Kuwa
ndio makao makuu yake. Hapo ilijengwa studio kubwa, office na apartment
za kuishi kadhaa. Mwaka 1978 alitiwa mbaroni tena baada ya kugundulika
kuwa alikuwa anasambaza nyimbo zenye matusi ambazo hakuzipitisha
katika kamati ya kuchunguza mashahiri kama ilivyokuwa kawaida wakati
ule. Kufikia kipindi hiki TPOK Jazz ilikuwa kubwa kiasi iliweza
kumeguka kuwa mbili moja ikifanya kazi Afrika wakati nyingine ikiwa
inafanya maonyesho Ulaya. !983 Franco alifanya maonyesho kadhaa Marekani
lakini hayakufanikiwa haijajulikana mpaka leo sababu za kushindikana
huko. Katikati ya miaka ya 70 Franco alibadili dini na kuwa Muislam na
kupewa jina la Abubakkar Siddiki, japo hakuonekana kufuata taratibu
zozote za Kiislamu na akaendelea kuitwa Franco. 1980, Franco alitajwa
kama ndie Grand Master wa muziki wa Kongo na serikali yake, ghafla na
nyimbo zake nyingi zikaanza kuwa zinasifia utawala ulikuweko madarakani.
1985 Franco alitoa wimbo ambao uliuza kuliko nyimbo zake zote
, Mario, ambao ulikuwa ni hadithi ya mwanaume kijana ambae
alikuwa anategemea akina mama watu wazima wamlee. !987 zilianza habari
kuwa Franco anaumwa sana, na kwa mwaka ule alitoa wimbo mmoja Attention Na SIDA
(Jihadhari na UKIMWI), wimbo huu ukaanzisha maneno kuwa pengine Franco
kasha upata ugonjwa huu. Franco akawa taratibu anakosekana kwenye
shughuli za bendi nayo ikaanza kumeguka kutokana na kutokuwa na uongozi
thabiti. Franco tena akarudi kwenye dini yake ya awali ya Roman
Catholic. Tarehe 12 Oktoba 1989, Franco alifariki katika hospitali moja
Ubelgiji. Mwili wake ukarudishwa Kongo, sanduku likiwa limefunikwa
bendera ya Taifa lake na kupitishwa katika mitaa ya Kinshasa na kuagwa
na maelfu ya wapenzi wake. Serikali ikatangaza siku 4 za maombolezo
ambapo redio ya serikali ilipiga nyimbo za Franco tu. Franco alizikwa
tarehe17 Oktoba 1989. Alifariki akiwa na miaka 51. Mumgu amlaze pema
peponi
habari:kitimeblog
No comments:
Post a Comment