ndikumana kuandaliwa fumanizi
Baada
ya Uwoya kufunguka namna mwanamke huyo (shoga’ake) alivyomuibia ‘mali’
zake katika gazeti pacha la hili, Ijumaa toleo namba 755 la Januari 6
hadi 12, 2011, inadaiwa kuwa Janeth alipata wakati mgumu kutokana na
mume wake kuhitaji majibu ya kueleweka na kusababisha ndoa yake kuwaka
moto.
Katika habari hiyo, Uwoya alitamka laivu kuwa aliwafuma Janeth
na Ndikumana katika mazingira ambayo huhitaji kuambiwa kwani kama hujui
kusoma, hata picha huwezi kuangalia?
MAANDALIZI YA FUMANIZI
Kwa
mujibu wa mtu wa karibu wa familia ya Janeth, kuna kila dalili endapo
Ndikumana ataendelea ‘kumsumbua’ mwanamke huyo kama alivyodai, ipo
mikakati kabambe ya kutokea fumanizi la kihistoria.
“Ninavyomjua mume
wa Janeth ana wivu sana kwa mkewe, lazima atamwekea Ndikumana mtego wa
fumanizi ili amuaibishe,” kilisema chanzo chetu.
IJUMAA WIKIENDA KULETEWA PICHA ZA FUMANIZI
“Ni
kiasi cha kumwambia Janeth amkubalie tu ‘then’ wakiingia chumbani,
wanavamiwa na kupigwa picha, msijali zitaletwa kwenu (Ijumaa Wikienda),
mtaziona na mtakuwa wa kwanza kuripoti.”
KWANI JANETH AMEOLEWA?
Kuhusu
kuwa na ndoa yake, tena mbichi, Janeth alifunguka: “Jamani nina ndoa
yangu, nimeolewa mwaka jana kule Madagascar ninakoishi na mume wangu
ambaye ni raia wa Kongo-DRC. Kwa sasa nipo Dar kwa mapumziko, lakini
baba watoto ni mfanyabiashara ‘so’ yupo Burundi na Rwanda kikazi.”
HALI ILIKUWAJE BAADA YA UWOYA KUCHAFUA HALI YA HEWA?
“Mume wangu alipata habari na wengine walimpelekea gazeti ‘so’ amekasirika sana, kaniambia anakuja Dar sijui hata itakuwaje.
“Nilipokea
simu nyingi sana, kuna mtu aliniambia Irene (Uwoya) ananitafuta, yaani
Bongo imenishinda, ngoja nirudi zangu Madagascar kabla hayajanikuta
makubwa kwani namjua mume wangu alivyo mkali.”
BADO HALI SI SHWARI
Hivi
karibuni Uwoya na Ndikumana waliingia kwenye gogoro zito huku ndoa yao
ikidaiwa kutibuka ambapo hadi sasa hali bado si shwari.
chanzo;gpl
No comments:
Post a Comment