JESHI
la Polisi mkoani Lindi wakishirikiana na askari wa kupambana na kuzuia
madawa ya kulevya kutoka jijini Dar es salaam, wamekamata jumla ya kilo
210 za madawa ya kulevya aina ya Heroine, yanayokadiliwa kuwa na thamani
ya Sh, 6.3 bilioni.
Kaimu kamanda
wa Polisi mkoani hapa, George Mwakajinga amewaambia waandishi wa habari
hizi Ofisini kwake mjini hapa kuwa, madawa hayo yamekamatwa jana,saa
12:0 asubuhi, katika kijiji cha Mchinga mbili, wilaya ya Lindi.Amewataja
waliokamatwa kuwa ni pamoja na mwenye nyumba yaliyokutwa madawa hayo,
aitwae Pendo Mohamedi Cheusi (67) mkazi na mkulima wa kijiji hicho na
Hemedi Said (27) dereva na mkazi wa mtoni,jijini Dar es salaam,ambaye
pia ni mtoto wa mwenye nyumba yaliyokutwa madawa hayo.
Wengine
ni Isumaili Adamu kwa jina lingine Athuman Mohamedi Nyaubi (28)
mfanyabiashara wa magari nchini Afrika ya kusini na mkazi wa Moroko
jijini Dar es salaam na Morine Amatus (22) mkazi wa Mikocheni ‘B’ pia
jijini Dar es salaam.
Mwakajinga
amesema madawa hayo yamekamatwa ndani ya nyumba ya Pendo Cheusi,yakiwa
yamehifadhiwa ndani ya madumu yapatayo manane yaliyokuwa na ujazo wa
lita 60 kila moja,tayari kusafirishwa kupelekwa nje ya nchi.
Amesema
mafanikio ya kukamatwa kwa madawa hayo,yamechangiwa na raia wema kutoa
taarifa za siri ndani ya Jeshi hilo ,kisha kufanikisha kuyakamata.“Sisi
Polisi kwa kushirikiana na kikosi kazi kilichokuwa kinaongozwa na mkuu
wa upelelezi mkoa wa Lindi,ASP,Faustine P.Hokororo,walipofuatilia
hatimaye jana tumefanikiwa kuyashika madawa hayo wakiwemo na wahusika”
Alisema Mwakajinga.
Mwakajinga
amesema tayari madawa hayo, yamesafirishwa kupelekwa jijini Dar es
salaam , kwa mkemia mkuu kwa ajili ya kuyapima, sanjari na kuyatunza
wakati kesi ya watuhumiwa hao itakapokuwa ikiendelea
mahakamani.Kaimu
kamanda huyo amesema watuhumiwa wawili kati ya wanne walioshikwa
wamefiishwa mahakamani leo ambapo upelelezi zaidi ya madawa hayo
ukiendelea.Pia Mwakajinga amewashukuru wale wote waliofanikisha kutoa
taarifa ya kuwepo kwa madawa hayo, na kuongeza ni mara ya kwanza kwa
mkoa wa Lindi kukamata madawa mengi kiasi hicho, huku akizidi kuwaomba
wananchi
kuendelea kushirikiana na vyombo vya dola kutoa taarifa pale
wanapobaini kuwepo kwa vitendo ambavyo vinakwenda kinyume na maadili ya
nchi.
No comments:
Post a Comment