Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dkt. Ramadani Dau akifafanua mambo juu ya utekelezaji wa Mradi wa Daraja la Kigamboni
Mkurugenzi
Mkuu wa NSSF, Dkt. Ramadhani Dau akitia saini ya kama ishara ya kuanza
Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni kulia ni Mkurudenzi Mtendaji wa
Kampuni ya China Railway Jiang Engineering CO. LTD, Shi Yuan.
Serikali
kupitia Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), leo imetia saini
na Kampuni ya Kichana, China Railway Jiangchang Engeneering CO. Ltd kama
ishara ya kutekeleza ujenzi wa mradi wa daraja la Kigamboni
utakaogharimu zaidi ya Shilingi bilion 214.6 kwa muda wa miezi 36.
Akizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dkt. Ramadhani Dau, alisema Shirika la NSSF itachangia asilimia 60, wakati serikali itachangia asilimia 40.
“Kunakila
sababu ya kukamilisha mradi wa daraja kwa wakati hii nikutokana na
kuwepo tayari kwa pesa za mradi, ni matumaini yangu mradi utafanikiwa
kwa wakati na watanzania kushuhudia ndoto ya ujenzi wa daraja
imekamilika” alisema
Alisema
licha ya kusaini mkataba huu kama ishara ya kuanza kwa mradi zipo
changamoto nyingi lakini baadhi ya changamoto ni kwa upande wa kurasini
kuna kiwanja kinjamatatizo, vile vile baadhi ya makutano ya barabara ya
Chang’ombe , Kamta na Tazara ktuokana na foleni kubwa lakini haya yote
tunaimani serikali itayapatia ufumbuzi wa haraka.
Naye
Waziri wa Ujenzi, Dkt. Magufuli amewataka wahandisi ambao wamechukuwa
tenda hiyo kufanyakazi kwa kiwango kinacho kubalika na kwa wakati,
“Kutimia kwa mradi ni miezi 36, hii ni kwa makadirio ya
juu lakini mradi unaweza kukamilika chini ya miezi 36, hivyo hakuna
haja ya kusubiri muda wote ikiwa pesa ya maradi ipo” alisema
Kwa
upande wake Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudencia Kabaka, almetoa rai kwa
watanzania kutumia fulsa ya ajira itakayo jitokeza kwa kwa kipindi hicho
chote cha utekelezaji wa mradi,
“Kwa
taarifa zilizonifikia kutoka kwa wataalamu wa mradi kuwa kutakuwa na
ajira za kudumu 1000, na za muda mfupi 2000, hivyo watanzania tutumie
hizo fulsa za ajira kufanya kazi kwa ufanisi na uaminifu kwa maslahi ya
Taifa” alisema Kabaka\
picha na habari kwa niaba ya fullshangweblog
No comments:
Post a Comment