NYUMBA HIYO INAYODAIWA KUPANGWA NA BILIONEA
Kila kitu cha Wema Sepetu kimebadilika, mambo yake kwa sasa yapo juu
ya mstari baada ya bilionea mkubwa Dar (jina tunalo) kudaiwa kujitosa
kumlea mrembo huyo akianzia kwa kumpangishia nyumba ya kifahari.
Habari kutoka kwa vyanzo vyetu zinadai kuwa bilionea huyo
amempangishia Wema nyumba hiyo eneo la Makumbusho, Kijitonyama, Dar es
Salaam.
“Wema ni binti mrembo mwenye mvuto wake, ukizingatia ana nyota pia ya
kupendwa, kwa hiyo siyo mtu wa kukaa na kukubali kufujwa mpaka azeeke,”
alisema mtoa habari wetu ambaye ni ‘shostito’ wa Wema na kuongeza:
“Mtu na hela zake ameingia kwa presha kubwa, ameahidi kumpa matunzo
ya nguvu. Mbali na kumpangia nyumba, ameahidi pia kumnunulia gari la
kutembelea.”
Chanzo chetu kingine kilipasha kuwa Wema kwa sasa amekata shauri la
kuacha kujihusisha na mapenzi ya vijana wadogo kwa sababu wengi wao
wanakuwa hawajaamua kutulia kufanya maisha.
“Hata sisi wenyewe kama marafiki zake tumemuunga mkono na tumemshauri
azingatie hilo. Unajua inauma sana kupoteza muda kuwekeza upendo wako
kwa mtu ambaye hana mapenzi au mtu ambaye bado anawaza kurukaruka.
“Hayo ndiyo ambayo Wema ameyatafakari na anajutia muda wake ambao
aliupoteza kwenye mapenzi yasiyo na uelekeo,” kilisema chanzo chetu.
Kwa mujibu wa vyanzo vyetu, Wema ameamua kuanza upya kwa kila kitu
ili kutibu majeraha ya moyo aliyoyapata baada ya kuachana na aliyekuwa
mchumba wake, Naseeb Abdul ‘Diamond’.
Utata kuhusu mahali ambapo Wema amepata fedha za kupanga nyumba, upo
hata kwa mama yake mzazi, Mariam Sepetu ambaye aliliambia Amani kuwa
ameshindwa kumbana kwa sababu ni binti mkubwa hivi sasa.
“Wema aliposema anapanga, mimi na mjomba wake tulimuweka chini
atuambie uwezo wake wa kupanga nyumba, fedha amepata wapi na amejipanga
vipi kuendesha maisha ya kujitegemea.
“Alitujibu kwamba anapanga nyumba mwenyewe. Tulimkatalia na kumtaka
aishi nyumbani lakini alikataa kwa maelezo kuwa hawezi kuishi nyumbani
miaka yote kwa sababu amekua. Tumemkubalia na mimi mama yake nimeshindwa
kumbana zaidi kwa sababu amekua,” alisema Mariam.
Jitihada za mapaparazi wetu kumpata Wema atie neno kuhusu ‘mchanyato’
huo, ziligonga mwamba, kwani simu yake ilikuwa haipatikani na hata
alipofuatwa nyumbani kwake mara nne kwa siku mbili mfululizo hakuwepo.
Wema, ameanza maisha mapya ya kujitegemea baada ya kuwekana kando na aliyekuwa mchumba wake, Diamond.
CNAZO:GLOBALPUBLISHERS
No comments:
Post a Comment