Na Sifael Paul
Habari za kuaminika zinadai kuwa staa mkubwa wa filamu za Kibongo ambaye ni
mshikiliwa wa kwanza katika kesi ya kifo cha Steven Charles Kanumba ‘The Great’,
Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameokoka, Risasi Jumamosi linafunguka.
Kwa mujibu wa mmoja wa waumini 53 wa Kanisa la Efatha Foundation Tanzania
lililopo Mwenge, Dar es Salaam linaloongozwa na Nabii Josephat Mwingira, Lulu
aliombewa na ‘kondoo’ hao wa Mungu wakati akiwa nyuma ya nondo za mahabusu ya
Kituo cha Polisi cha Oysterbay, Kinondoni.
Chanzo hicho cha habari kilidai kuwa, waumini hao walijikuta wakimwongoza
staa huyo sala ya toba huku nao wakiwa na ‘kimeo’ baada ya kufikishwa kituoni
hapo wakidaiwa kuhusika kwenye msala wa vurugu na kutaka kubomoa majengo ya
kiwanda cha uchapaji cha Afro Plus kilichopo jirani na kanisa lao.
“Ilikuwa Jumatatu ya Pasaka, habari za kifo cha Kanumba zilikuwa
zimeshika kasi katika kila kona, tulipopelekwa mahabusu ya Oysterbay ndipo
tukamkuta Lulu. Ukweli ni kwamba aliongozwa sala ya toba na waumini akitamka
mwenyewe: “Eee Mungu… naomba ulifute jina langu kwenye kitabu cha
hukumu…liandike katika kitabu cha uzima wa milele…Ameni.” Alisema mtoa habari
huyo.
Wakati huohuo, habari za ndani kutoka lupango Segerea alikowekwa
Lulu zilidai kuwa katika siku za karibuni amekuwa kama kachanganyikiwa huku
akifanya vitu tofauti ikiwemo kucheza kiduku mara kwa
mara.
chanzo:GPL
No comments:
Post a Comment