RPC wa Kinondoni-Charles Kenyela |
POMBE kali (Whisky) aina ya Jacky Daniel, imetajwa kama chanzo cha kifo cha mwigizaji nyota wa filamu nchini, Steven Charles Kanumba aliyefariki usiku wa kuamkia jana nyumbani kwake, Sinza, Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Kinondoni, ACP Charles Kenyela amesema leo kwamba uchunguzi wa awali unaonyesha hivyo, lakini bado wanaendelea na uchunguzi zaidi, ili kujua zaidi.
ACP Kenyela amesema kwamba Kanumba wamefanikiwa kumuhoji mtuhumiwa wa kwanza katika tukio hilo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na katika maelelezo yake amekanusha kumsukuma Kanumba.
Vyombo vingi vya habari vilimnukuu ndugu wa Kanumba, Sethi jana akisema kwamba Lulu alimsukuma mwigizaji mwenzake huyo katika ugomvi wao wa wivu wa kimapenzi hadi akaanguka na kufariki dunia.
Akizungumza kutokana na maelezo ya Lulu, Kamanda huyo alisema kwamba; ugomvi wao ulitokana na Kanumba kutaka kumdhibiti Lulu wakati akizungumza na simu.
“Kanumba aliamua kumfuata Lulu nje huku akifoka kwa sauti, akitaka aelezwe kwa nini alitoka nje kupokea simu, huku akimtuhumu kuwa huenda alikuwa akizungumza na mwanaume mwingine.
Baada ya Lulu kuona Kanumba anamfuata, aliamua kukimbia kutoka nje ya geti, lakini kabla hajafanikiwa kufungua geti, Kanumba alimkamata na kumrudishwa ndani. Kanumba akiwa amemshikilia, waliingia wote chumbani na kufunga mlango. Sasa haijulikani nani aliyefunga mlango, ingawa maelezo ya Lulu, anadai kuwa aliyefunga mlango ni Kanumba,”alisema Kamanda huyo.
Akiendelea kumnukuu Lulu, Kamanda huyo anasema; “Baada ya Kanumba kufunga mlango, alimuona akilegea na kujigonga kisogo chake kwenye ukuta wa chumba hicho kabla ya kuanguka chini,”alisema.
Alisema uchunguzi wa tukio zima ukikamilika, hatua inayofuata ni kumpeleka Lulu mahakamani kama mtuhumiwa wa mauaji.
Chanzo:http://mrokim.blogspot.com
No comments:
Post a Comment