Wednesday 2 May 2012

DIAMOND NA SHOW YA HELICOPTER

Stori: Waandishi Wetu
Ukizungumzia mapinduzi ya burudani Bongo, haijawahi kutokea shoo kama aliyoifanya mwanamuziki namba moja kwa sasa, Naseeb Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz’ akitumia helikopta, Risasi Mchanganyiko lina ripoti kamili ya kilichotokea nyuma ya pazia.
Shoo hiyo ambayo ni ya kwanza kufanyika Bongo ikiwa tofauti na zilizowahi kufanyika katika miongo kadhaa iliyopita, ilijiri ndani ya ukumbi bora wa burudani wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar wikiendi iliyopita, Aprili 29, mwaka huu.
Katika tukio hilo lililoshuhudiwa na waandishi wetu, siyo siri, maandalizi yake yalikuwa ya hali ya juu kuanzia helikopta iliyomsafirisha Diamond kutoka Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere hadi ukumbini, Dar Live.
Ilifahamika kuwa vazi alilovaa Diamond ambalo lilibuniwa na mwanamitindo ambaye ni laazizi wake wa sasa, Jokate Mwegelo lilizua gumzo kwani mashabiki walilifananisha na la kijeshi.

ATUA KAMA MJESHI
Tukio hilo lilikuwa kama bonge la muvi lakini haikuwa hivyo bali lilikuwa la kweli.
Kabla ya kutua kwenye Uwanja wa Zakhem Mbagala, Diamond alizunguka mara kadhaa angani na kusababisha mtikisiko mkubwa kwa wakazi wa Dar waliokuwa wakishangilia na kukimbilia upande ilikokuwa ikielekea helikopta iliyombeba staa huyo.
Akiwa mita mia moja angani usawa wa jukwaa linalopanda na kushuka la Dar Live, kabla ya kutua, Diamond alitumia ‘maiki’ aliyokuwa nayo kwenye helikopta kutoa vionjo vya nyimbo zake huku umati uliokuwa chini ndani na nje ya ukumbi huo ukimuitikia kwa vifijo na mayowe.
Baada ya kutoa vionjo hivyo akiwa angani, ndipo helikopta hiyo ilipotua kwenye Viwanja vya Mbagala Zakhem na Diamond akashuka kisha kutoa saluti kwa marubani wa helikopta hiyo kabla ya kuingia kwenye gari maalum aina ya Mercedes Benz Compressor.
Baada ya tukio hilo, mwanamuziki huyo alikwenda kujipumzisha kwenye Hoteli ya Johannesburg, Sinza kujiandaa na shoo huku akisindikizwa na king’ora na difenda la polisi.

DIAMOND AFANAFANYA SHOO ‘KLASIKI’
Ndani ya Dar Live, moto wa burudani ulianzishwa na Joseph Gabriel Rushahu ‘Bwana Misosi’, Maunda Zorro, Timbulo Ally kisha wasanii kutoka Afrika Kusini wanaotamba na traki zao za You na Amatita wanaounda Kundi la Pah One, walimkaribisha Diamond ambaye alifanya shoo ‘klasiki’ na ya kihistoria.
SHOO YA UTANGU LIZI
Rais huyo wa Wasafi alipofika ukumbini tayari kwa shoo, filamu fupi (documentary) ya kushuka kwa helikopta ilioneshwa kupitia ‘skrini’ kubwa zilizopo ukumbini hapo.
Wacheza shoo wake ambao nao walivalia sare kama za kijeshi na mabuti makubwa, walilivamia jukwaa kwa shoo fupi kisha Diamond akaingia kudondosha shoo kali kupitia ngoma zake.
NIZAI DI YA SHOO
Wakati ‘kichaa’ huyo wa Bongo Fleva anayeshikilia tuzo tatu za Kili 2012 akiwa stejini, alikuwa akishangiliwa kwa mayowe kuanzia mwanzo wa shoo hadi mwisho.
Shoo ya jamaa huyo ilikuwa ya kipekee kwa sababu alifanya makamuzi ya kiburudani kwa takribani saa tatu mfululizo bila kusimama (non-stop) huku yeye na madensa wake wakibadili nguo kwa awamu mbili tofauti.
Baada ya shoo, Diamond aliyeambatana na mama yake, Sandra aliwashukuru mashabiki wote ambao hawakujali mvua iliyodondoka na badala yake wakajirusha vilivyo na kusuuza nyoyo zao.
KWA NINI HAI JAWA HIKUTOKEA?
Historia miaka ya nyuma inaonesha kuwa mwanamuziki mkongwe wa dansi Bongo, Ali Choki aliwahi kutangaza kushuka na helikopta katika uzinduzi wa albamu yake ya Bullet Proof kwenye Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni lakini ilishindikana.
Achana na Ali Choki, wapo wasanii wengine wakongwe katika gemu kama Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Nice Lucas Mkenda ‘Mr Nice’ ambao walifikia hatua kubwa za kimaendeleo ya kimuziki lakini hawakuwahi kushuka na helikopta jukwaani na kugonga shoo kama aliyofanya Diamond.
Kigezo kingine ni maelfu ya watu waliojitokeza kumpokea Diamond ukumbini hapo ambao walisema shoo hiyo ni ya kwanza katika historia yaburudani kutokana na hadhi ya juu kuanzia maandalizi, mapokezi hadi shoo yenyewe.
NENO LA RISASI MCHANGANYIKO
Huu ni mwaka wa Diamond kimafanikio, ameshinda tuzo tatu za Kili 2012, shoo yake ya pale Mlimani City ilitikisa na sasa ametengeneza historia ya kushuka na helikopta Dar Live. Ni wakati wake kujipanga zaidi kuhakisha hashuki na anazidi kwenda juu kimaendeleo.

NB
SHOW ILIKUA NZURI NDIYO LAKINI KUNA FIX HAPA,MAANA HAIKUFIKA MASAA MATATU AKITUMBUIZA,SANA SANA ILIKUA LABDA SAA 1:30 NDIO ALIKUA LIVE PALE JUKWAANI WAANDISHI ,TUJARIBU KUWA WAKWELI

No comments:

Post a Comment