Ghasia zimekumba mji mkuu wa
Tanzania Dar es Salaam kufuatia maandamano kuhusiana na kukamatwa kwa
kiongozi wa dini ya kiislamu sheikh Ponda Isa Ponda.
Waumini wa dini hiyo wamekabiliana na polisi punde tu baada ya sala ya ijumaa.Mwandishi wa BBC mjini humo Eric David Nampesya alisema kuwa polisi walitumia gesi ya kutoa machozi ili kuwatawanya watu kadhaa waliokuwa wamekusanyika wakitishia kuandamana hadi katika eneo la Kidongo Chekundu kudai malalamiko kadha wa kadha.
Kikosi cha jeshi la polisi kilishirikiana na polisi mjini Dar Es Salam kukabiliana na waandamanaji waliokuwa wamesema watafanya maandamano baada ya sala ya Ijumaa.
Sheikh Ponda alikamatwa kwa madai ya uchochezi.
Polisi walitumia gesi ya kutoa machozi kutawanya makundi ya vijana waliokuwa wanafanya vurugu.
Afisa mmoja wa polisi aliuawa katika ghasia zilizofanyika siku ya Jumatano baada ya taarifa za kutoweka kwa sheikh Adi kutolewa. Polisi wamewakamata watu kadhaa kuhusiana na vurugu hizo.
BBCSWAHILI
No comments:
Post a Comment