Akizungumza na kituo kimoja cha redio cha jijini…
Na Sifael Paul
HUKU mumewe akiwa amezikwa Jumatano iliyopita kijijini kwao Kilema,
Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro, mke wa aliyekuwa Kamanda wa Polisi wa
Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow (53), aliyeuawa na watu waliosadikiwa
kuwa ni majambazi wiki iliyopita, amefunguka neno la mwisho
alilozungumza na baba watoto wake huyo kabla ya kukutwa na umauti,
Ijumaa linakujuza.
Akizungumza na kituo kimoja cha redio cha jijini Dar es Salaam, juzi
huku akiangua kilio kwa uchungu, mke huyo wa marehemu ambaye walijaliwa
watoto watatu alisema kuwa mara ya mwisho mumewe alimwambia kuwa
anakwenda kwenye kikao cha harusi ya ndugu yao na hayo ndiyo yalikuwa
mazungumzo yao ya mwisho.
Huku akishindwa kuzungumza vizuri kutokana
na maumivu ya kuondokewa na mwenza wake huyo, mama huyo alisema maneno
hayo ndiyo yalikuwa ya mwisho kuzungumza na muwewe hadi alipopata
taarifa ya kifo hicho ambapo mwanzo ilikuwa vigumu kuamini.
Alisema
kwa upande wake anaamini serikali kupitia Jeshi la Polisi nchini
itafanya kazi yake hivyo hakutaka kuongeza neno kwani uchunguzi wa
mauaji hayo unaendelea na kila kitu kitajulikana utakapokamilika.
Kamanda Barlow aliuawa usiku wa Oktoba 13, mwaka huu eneo la Kitangiri,
Mwanza kwa kupigwa risasi na watu hao waliokuwa wamevaa w w makoti
yanayovaliwa na vijana wa ulinzi jamii.
gpl
No comments:
Post a Comment