Monday 8 October 2012

WACHINA WADAIWA KUIHUJUMU TANESCO

 
Na: Kelvin Matandiko, Mwananchi. 

KAMPUNI ya kichina inayojishughulisha na utengenezaji wa Magari chakavu iitwayo ‘China Tanzania Garage Enterprises Ltd’ imedaiwa kulihujumu Shirika la Umeme nchini (Tanesco) kwa kuiba umeme katika kipindi cha miaka kumi. 

Kampuni hiyo ya kichina ambayo kwa sasa imehamishia shughuli zake mitaa ya Mikocheni,o inadaiwa kutumia umeme wa Tanesco kwa njia ya wizi kupitia uharibifu wa mashine ya luku na kuunganisha nyaya katika kipindi chote walichokuwa hapo. 


Akizungumza mama mwenye nyumba hiyo ,Laurensia Roman, alisema Wachina hao walipanga kwa kipindi cha miaka kumi katika nyumba yake kwa shughuli za utengenezaji wa magari bila kutambua kama kulikuwa na wizi uliokuwa unafanywa na wachina hao. “Wamehama mwezi Juni mwaka huu bila hata kunijulisha,wameondoka na deni la miaka mitatu la kodi ya nyumba na kuhamia mikocheni,sikujua chochote kile juu ya utapeli wao,”alisema Laurensia. 


Katika tukio lingine mitaa hiyo ya Sinza kwa Remi, Tanesco kupitia operesheni hiyo maalumu kwa kanda ya Kinondoni Kaskazini,ilifanikiwa kukata umeme katika nyumba nne ikiwamo hoteli ya ‘City fast food’ baada ya kubainika na kosa la kuchezea mita. Baada ya kuzungumza na Meneja msaidizi wa hoteli hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Balozi Ntashogelwa, alisema Tanesco imefanya makosa kukata umeme katika hoteli yake kwani ilipaswa kutoa taarifa kabla ya kwenda kufanya ukaguzi huo. 


“Sasa jamani mimi nitafanyaje sasa wamekata umeme ,vyakula vyote viko kwenye friji, kwa nini hawakuja kutoa taarifa mapema,hii hasara itakayopatikana mimi nitafanyaje,”alilalamika Ntashogelwa.

 Ofisa usalama na kiongozi wa kikosi cha ukaguzi wa mita za luku katika kanda ya Kinondoni kaskazini, Dunia Shami alisema msimamo wa Tanesco ni kuhakikisha wateja wote wanakuwa waaminifu na kwamba wataendelea na operesheni hiyo ya kushtukiza ili kuwakamata wasiokuwa waaminifu. 
                                                            Mwanachi

No comments:

Post a Comment