Tuesday 29 January 2013

Mwenyekiti mpya Chadema kupatikana Desemba 13




Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika akizungumza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya chama hicho Dar es Salaam jana. Kulia ni Ofisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene. Picha na Joseph Zablon. 

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetangaza ratiba ya uchaguzi wake wa ndani, inayoonyesha kuwa kitapata mwenyekiti mpya ifikapo Desemba 13, mwaka huu.
Ratiba iliyotolewa na chama hicho Dar es Salaam jana imeeleza kuwa uchaguzi huo wa mwenyekiti, utatanguliwa na chaguzi nyingine za ngazi za majimbo, mkoa, wilaya, kata na tawi.
“Uchaguzi utaanza Aprili, mwaka huu na tunatarajia umalizike Desemba mwaka huu kwa kumchagua mwenyekiti taifa,” alisema Mkurugenzi wa Habari na Uenezi, John Mnyika.
Alisema kuanzia Aprili hadi Septemba kutafanyika chaguzi katika ngazi za msingi ambazo zinajumuisha matawi, majimbo na wilaya kabla uchaguzi huo haujafanyika katika ngazi ya mkoa kuanzia Novemba.
“Uchaguzi ngazi ya taifa utahusisha pia jumuiya za chama ambazo ni Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Baraza la Vijana (Bavicha), Wazee, Kamati Kuu na Baraza Kuu Taifa,” alisema.
Nafasi nyingine zitakazoshindaniwa ni za wajumbe wa mkutano mkuu wa taifa.

mwananchi

No comments:

Post a Comment