Friday 4 July 2014

Mwanamke mbaguzi achunguzwa Australia

australia
Bbcswahili
Polisi nchini Australia wanamchunguza mwanamke anayedaiwa kuwatusi abiria wenzake matusi ya kibaguzi mjini Sydney.
Aliwatukana akitumia ishara za kibaguzi, akiwakemea kuhusu lafudhi zao na kumtaja mwanamke mmoja kuwa 'Gook'
Mmoja wa abiria waliokuwa kwenye treni hiyo alimnasa mwanamke huyo akitoa matusi hayo kwa kutumia simu yake kisha kuiweka kanda hiyo kwenye mtandao wa Youtube.
Kanda hiyo ya dakika tatu na nusu, imejaa matusi ya kibaguzi tu.
Iliwekwa kwenye mtandao wa Youtube, Jumatano, na mmoja wa abiria waliokuwemo ndani ya treni hiyo.
Kanda hiyo inaanza kwa mwanamke huyo kueleza hasira yake kwa watoto ambao walikataa kumsimamia ili aweze kuketi.
Kisha akaanza kumtukana mwanamke aliyemuita mtu wa Asia' pamoja na mwanamume aliyedhani alikuwa mpenzi wa mwanamke huyo.
Mwangalieni huyu 'bogan' hapa,'' anasema mwanamke huyo, akitumia lugha ya mtaa ya Australia ambayo ni sawa na kusema 'takataka'. Unaweza kupata tu 'gook', huna uwezo wa kupata msichana wa kaiwada? alimuuliza mwanamume aliyekuwa ameketi na mwanamke huyo. Nina kuhurumia sana wewe 'gook' . Neno Gook hutumika kumkejeli mtu na lilitumika wakai wa vita vya Vietman.
Kanda hiyo imetazamwa zaidi ya mara 150,000 kwenye Youtube pamoja na mjadala kwenye Twitter na Facebook kuhusu ubaguzi wa rangi.
Chini ya sheria za Australia kuhusu ubaguzi, ni kinyume na sheria kumuudhi mtu , kumtukana, kumadhalilisha na hata kumtisha kwa sababu ya rangi yake au kabila lake.
Lakini serikali kwa sasa inajadili ikiwa itafutulia mbali kipengee hicho .Mpago huo ni tatanishi, na baadhi wamezungumzia sheria hiyo katika mjadala.
Baadhi ya watu wamemtetea mwanamke huyo wakisema kuwa wahamiaji wamejaa Australia na wanjidai sana utadhani huko ndio kwao.
Lakini wananchi wengi wa Australia waliomba msamahakwa niaba ya mwanamke huyo.
''Mwanamke huyo hawakilishi maoni ya watu wa Australia, pole kwa walioudhika sana na ni aibu sana kwetu,'' walisema watu wengi nchini humo.

Mwanamke huyo anajulikana kama Sue Wilkins, mwenye umri wa miaka 55 na inaarifiwa aliomba msahama kwa matamshi yake na kusema kuwa alikosa sana.

No comments:

Post a Comment