du huyu msoja hata akipewa denda anaweza kummeza mkewe hilo domo
unakumbuka enzi ya chipukizi?akumbuka enzi hizo maana tulikua tukimaliza shule jioni lazima ukahudhurie mafunzo ya chipukizi(CCM bana)nilikuwa naitwa afande nanihii,maana kupata uafande ilikua shughuli nzito.lazima uonyeshe ushujaa wako wa ugumu wa kukabiliana na vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja na maisha.kulikuwa na kipindi mnaenda ishi maporini juu ya miti sometime,lakini nashukuru mungu ilisaidia nilipaona chekslovakia miaka hiyo.nilienda huko kwaajili ya skauti na ndio niliporudi nikapewa uafande chipukizi.skauti ilikuwa ni kama jeshi.maana mnajifunza jinsi ya kuishi katika mazingira tofauti na watu tofauti,leo hii inasaidia katika maisha haya.kipindi cha uafande chipukizi nilikuwa naogopewa na hawa walio chini kiasi ambacho wakikuona wanakimbizana wenyewe.maana mtu akileta kujua unamtime muda wa paredi.muda huo atakula fimbo za mgongo huku anatembea kikakamavu mbele ya mgeni rasmi.ilikuwa hamna kughairi mgeni rasmi yuko mbele wee,basi nasisi maafande mradi visa tu unamtafuta mtu wako mda huo wa pared unampa mboko saafi,akimaliza pared unamwomba msamaha kwamba "eeh mshkaji sore si unajua nilikua kazini"sijui kama mambo haya yapo tena(skauti na chipukizi)
No comments:
Post a Comment