Tuesday 1 March 2011

MAMBO YA UBWII NA MIPAKAZO



John alipochoka kufanya kazi zake akazima taa, akambusu mkewe,
akalala na usingizi mzito ukampitia. Mara akamwona mwanamme amesimama

kitandani.

"Toka hapa nani wewe unakuja kitandani kwangu?"

"mimi ni mtakatifu Petro na hapa si kitandani kwako bali ni mbinguni"

"Ina maana nimekufa? Mbona mimi bado kijana? Naomba unirudishe duniani."

"Inawezekana, lakini siwezi kukurudisha kama mtu, labda nikurudishe kama mbwa au kuku"
John akakumbuka mbwa anavyopata taabu ya kulinda, "Bora nirudi kama kuku"

Mara akajikuta yuko kwenye banda, akiwa kuku jike na matakoni kunawaka

moto. Akamwona jogoo pembeni, akamwambia shida yake.

"Kaka ninasikia moto matakoni, inakuwaje?"

"Kwani hujawahi kutaga weye?" Jogoo akamjibu kwa maringo.

"Sijawahi"

"Chuchumaa, kamua kwa nguvu yai litoke."

Basi akakamua, yai la kwanza likatoka, akakamua tena yai la pili hilo!

Akiwa anataka kukamua yai la tatu akasikia sauti ya mke wake.

"John, pumbavu wewe, unakunya kitandani!"

No comments:

Post a Comment