Friday 20 May 2011

lunch time jana"UGALI DAGAA&BAMIA" enjoy


dagaa na bamia tayari

msosi tayari kwa kuliwa
mahitaji:

*dagaa kiasi
*bamia kiasi
*nyanya (kopo au fresh sawa)
*vitunguu vilivyokatwa katwa 1
*nazi tui(coco milk) 1
*cury powder(ukipenda)
*mafuta vijiko 2
*piri piri 1
*ndimu 1
*chumvi kiasi

matayarisho

weka mafuta yako kwenye sufuria yapate moto,kisha weka vitunguu na dagaa waliooshwa vizuri kwenye mafuta kaanga mpaka vitunguu na dagaa vianze kuwa brown,weka nyanya zilizokatwa au ya kopo huku ukigeuza geuza mpaka nyanya iive (dk5),kisha kamulia ndimu  weka  cury powder vijiko viwili,changanya kwa muda kidogo then weka nazi hapo na kama una youghout ya kupikia weka km huna pia poa tu nazi inatosha,weka bamia na maji kiasi na chumvi ya kutosha,tupia pilipili nzima(km unatumia)funika na acha ichemke pamoja mpaka uone mchuzi umekua mzito na dagaa wameiva.

tengeneza ugali na pakua mboga

baada ya hapo ungoje nini tena zaidi ya kufakamia?enjoy mdau

MTANISAMEHE WADAU HII MENYU ILIKUA JANA,LAKINI SI UNAJUA TENA BAADA YA KUTENGENEZA NIKAIFANYIA THEN NIKAJIKUTA NIMEPIGA MBONJI JUU YA KEYBOARD KWA AJILI YA KUVIMBIWA,LAKINI NIKAONA HAKIJAHARIBIKA KITU LEO MNAWEZA KUIPATA PIA




8 comments:

  1. Yam yam,udenda unanitoka.Dagaa uliwapata wapi? kama kuna mahali wanauza kwa hapa Sweden tafadhali nieleze.

    ReplyDelete
  2. Hakika huu ni uchokozi...haya kaka nawe nakutakia mlo mwema na ahsante kwa kutushirikisha.... naona niondoke hatraka hapa maana mate yanadondoka ovyoovyo:-)

    ReplyDelete
  3. he hee,poleni sana,da yasinta usinambie huna kafurushi cha dagaa hapo ulikoagiza toka bongo.
    edna dagaa wapo pale taj mahal pia hötorget chini kwenye duka la wapopo utapata

    ReplyDelete
  4. Asante sana nitawafuata huko waliko.

    ReplyDelete
  5. Kaka isack ilikuwa ni muda nilikuwa kunyumba na kila kitu nilichochukua kimekwisha ...na hapa nilipo hivyo vitu ni adimu muno...:-(

    ReplyDelete
  6. pole sana ila ni lazima ulale kwakweli maana ni kitamu alafu unajikuta unakula mpaka unalala hapohapo

    ReplyDelete
  7. pole sana ila ni lazima ulale kwakweli maana ni kitamu alafu unajikuta unakula mpaka unalala hapohapo

    ReplyDelete