dagaa na bamia tayari
msosi tayari kwa kuliwa
mahitaji:
*dagaa kiasi
*bamia kiasi
*nyanya (kopo au fresh sawa)
*vitunguu vilivyokatwa katwa 1
*nazi tui(coco milk) 1
*cury powder(ukipenda)
*mafuta vijiko 2
*piri piri 1
*ndimu 1
*chumvi kiasi
matayarisho
weka mafuta yako kwenye sufuria yapate moto,kisha weka vitunguu na dagaa waliooshwa vizuri kwenye mafuta kaanga mpaka vitunguu na dagaa vianze kuwa brown,weka nyanya zilizokatwa au ya kopo huku ukigeuza geuza mpaka nyanya iive (dk5),kisha kamulia ndimu weka cury powder vijiko viwili,changanya kwa muda kidogo then weka nazi hapo na kama una youghout ya kupikia weka km huna pia poa tu nazi inatosha,weka bamia na maji kiasi na chumvi ya kutosha,tupia pilipili nzima(km unatumia)funika na acha ichemke pamoja mpaka uone mchuzi umekua mzito na dagaa wameiva.
tengeneza ugali na pakua mboga
baada ya hapo ungoje nini tena zaidi ya kufakamia?enjoy mdau
MTANISAMEHE WADAU HII MENYU ILIKUA JANA,LAKINI SI UNAJUA TENA BAADA YA KUTENGENEZA NIKAIFANYIA THEN NIKAJIKUTA NIMEPIGA MBONJI JUU YA KEYBOARD KWA AJILI YA KUVIMBIWA,LAKINI NIKAONA HAKIJAHARIBIKA KITU LEO MNAWEZA KUIPATA PIA
Yam yam,udenda unanitoka.Dagaa uliwapata wapi? kama kuna mahali wanauza kwa hapa Sweden tafadhali nieleze.
ReplyDeleteHakika huu ni uchokozi...haya kaka nawe nakutakia mlo mwema na ahsante kwa kutushirikisha.... naona niondoke hatraka hapa maana mate yanadondoka ovyoovyo:-)
ReplyDeletehe hee,poleni sana,da yasinta usinambie huna kafurushi cha dagaa hapo ulikoagiza toka bongo.
ReplyDeleteedna dagaa wapo pale taj mahal pia hötorget chini kwenye duka la wapopo utapata
Asante sana nitawafuata huko waliko.
ReplyDeleteKaka isack ilikuwa ni muda nilikuwa kunyumba na kila kitu nilichochukua kimekwisha ...na hapa nilipo hivyo vitu ni adimu muno...:-(
ReplyDeletepole sana ila ni lazima ulale kwakweli maana ni kitamu alafu unajikuta unakula mpaka unalala hapohapo
ReplyDeletedah kwakweli lazima ulale
ReplyDeletepole sana ila ni lazima ulale kwakweli maana ni kitamu alafu unajikuta unakula mpaka unalala hapohapo
ReplyDelete