SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda, amkubali rasmi barua ya kujiuzulu kwa Mbunge wa Igunga, Rostam Azizi (CCM) na kwamba, sasa wanamwandalia mafao yake kwa kipindi alichofanya kazi.
Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel, aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa barua ya Rostam ilifika kwa Spika Makinda Julai 19, mwaka huu na baada ya kuridhika na maelezo yake, amekubaliwa kujiuzulu na sasa wanajiandaa kumlipa mafao yake.
Jole alisema baada ya kupata barua hiyo, ofisi ya Bunge na kuridhika na sababu zilizotolewa na Rostam ilimshauri Spika kutangaza rasmi kuwa kiti cha ubunge wa Jimbo la Igunga kiko wazi.Hivi karibuni Rostam likwenda Igunda na kutangaa kujiuzulu ubunge na ujumbe wa halmashauri Kuu ya CCM.Kujiuzuru kwa Rostam kulifuatia mzozo mkubwa ndani ya CCM ikiwamo mkakati wa kujivua gamba ndani yua chama hicho.
Hata hivyo, Rostam alisema hajivui gamba bali anaang’atuka kutokana na kile alichokiita kuachana na siasa za kupakana matope ndani ya chama hicho Kikongwe.Jole alisema kuwa barua ya Rostam iliyoandikwa Julai 15, mwaka huu ilimfikia Spika Makinda Julai 19 ambaye baada ya kuridhika na maelezo yake alimwandikia barua Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kumjulisha kuwa atangaze kwamba Jimbo la Igunga liko Wazi.
Hata hivyo, Rostam alisema hajivui gamba bali anaang’atuka kutokana na kile alichokiita kuachana na siasa za kupakana matope ndani ya chama hicho Kikongwe.Jole alisema kuwa barua ya Rostam iliyoandikwa Julai 15, mwaka huu ilimfikia Spika Makinda Julai 19 ambaye baada ya kuridhika na maelezo yake alimwandikia barua Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kumjulisha kuwa atangaze kwamba Jimbo la Igunga liko Wazi.
“Spika aliipokea barua hiyo Julai 19 ingawa iliandikwa Julai 15 na baada ya spika kujiridhisha, Julai 20 alimuandikia Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kumjulisha juu kuwa nafasi ya jimbo hilo iko wazi,’’ alisema Joel.
Alisema kuwa Ibara ya 71 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano inampa nafasi mbunge kujihuzuru nafasi yake na kwamba, mbunge huyo alifuata Ibara hiyo pamoja na Sheria ya Uchaguzi namba 61 (3).
Alisema kuwa Ibara ya 71 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano inampa nafasi mbunge kujihuzuru nafasi yake na kwamba, mbunge huyo alifuata Ibara hiyo pamoja na Sheria ya Uchaguzi namba 61 (3).
“Ibara ya 149 (2) inaeleza kwamba mbunge atahesabiwa kuwa amejiuzuru wadhifa wake mara tu barua yake itakapowasilishwa katika ngazi husika, au kulingana na maelekezo yake, hivyo tangu wakati huo Rostam si Mbunge,’’ alifafanua Joel.Kwa taarifa hiyo maana yake wakati wowote utafanyika uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi ya mbunge wa jimbo hilo.
Kuhusu taratibu zitafuata baada ya taarifa hiyo ya Spika, Joel alisema kuwa hakuna taratibu nyingine zitakazofuata isipokuwa ni kutomhesabu Rostam kama mbunge wa Bunge hilo.
Tume ya uchaguzi
Hta hivyo, Mkuregenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), Rajab Kiravu lisema barua ya Spika haiajamfikia.
Lakinia akasema mara itakapofika, Nec itaifanyia kazi kwa kuandaa uchaguzi mdogo kwa ajili ya kujaza kiti hicho.
"Kama wameandika Julai 20, sio siku nyingi sana inawezekana bado ipo njiani... Ikitufikia tutaifanyia kazi kwa kuandaa uchaguzi," alisema Kiravu alipowasiliana na gazeti hili kwa simu hili.
Mkopo wa gari
Joel ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shughuri za Bunge, alisema Rostam atalipwa mafao ya miezi saba ambayo alikuwa amelitumikia Bunge la Kumi.“Ni kweli anastahili kulipwa mafao yake, kwa kipindi cha miezi aliyotumikia jimbo hilo kwa kuwa ameacha kwa hiari yake, lakini kuhusu suala la mkopo sisi hatuhusiki. Kama alikuwa na mkopo katika benki yoyote hiyo ni juu yake kwa kuwa Bunge halikopeshi mtu bali kumdhamini,’’ alisema.
Kuhusu gari la ubunge Jeol alisema kama Rostam alikuwa na mkopo wa gari atatakiwa kuurejesha au atanyang’anywa, lakini Bunge halihusiki kwa vile alikopa yeye binafsi.Kwa mujibu wa Joel, kitendo cha Rostam Kujiuzuru kwa hiari yake ni cha kwanza kutokea katika Bunge la Muungano.
Wakati Joel akisema kuwa hakuna mbunge aliyewahi kujiuzuru kwa utaratibu huyo, kumbukumbu zinazonyesha kwamba, aliyekuwa Mbunge wa Mpwapwa Alli Said Mtaki (TANU) alijiuzuru ubunge mwaka 1967 kwa hiari yake baada ya kutofautiana na Mwalimu Nyerere kuhusu Azimio la Arusha.
Mtaki ambaye alikuwa Naibu Waziri wa Ushirika kwa wakati huo, alipinga kitendo cha kutakiwa kukabidhi mali zake kwani alikuwa na nyumba moja ya ghorofa ambayo aliona si sahihi kuikana.Hata hivyo, mwanzoni mwa miaka ya 1980 aligombea nafasi hiyo katika jimbo hilohilo na akapita na kulitumikia kwa vipindi viwili kabla ya kuangaushwa na George Lubeleje mwaka 1990.
mwananchi
No comments:
Post a Comment