Na Imelda Mtema
Siku chache baada ya mume wa Irene Uwoya, Hamad Ndikumana ‘Kataut’ (pichani) kuondoka nchini, imeelezwa kuwa Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza ndiye aliyemshauri, Risasi Mchanganyiko linafunguka.
Kwa mujibu wa chanzo kilichokuwa jirani na nyumba aliyopangisha mwanasoka huyo wa Rwanda, maeneo ya Sinza-Madukani, Dar es Salaam, Ndiku aliwahi kumsimulia kuwa alikuwa alipokea ushauri wa kuondoka Bongo kutoka kwa kiongozi huyo ambaye alimwambia ni shabiki mkubwa wa wanandoa hao kuanzia kwenye soka (Ndiku) hadi filamu (Uwoya).
“Aliniambia Nkurunziza huwa anasoma sana habari zinazowahusu kwa sababu ni shabiki wao ndiyo maana aliwahi kuwaalika Burundi. Alimwambia akisoma habari za ndoa yake anasikitika hivyo arudi kwao Rwanda,” kilisema chanzo hicho cha uhakika.
Chanzo hicho kiliendelea kudai kuwa mwanzoni Ndiku aligoma kwa kuwa alitaka aondoke Bongo na familia yake au akiwa ameicha katika mazingira mazuri ndiyo maana alisita, lakini mara baada ya kusaini mkataba wa kuichezea Timu ya Rayon Sports ya Rwanda hivi karibuni, alikubaliana na ushauri huo kisha akarejea kwao.
Jitihada za kumpata Ndiku hazikuzaa matunda lakini taarifa zilisema kuwa wikiendi iliyopita aliichezea Rayon mchezo wa kwanza dhidi ya Marine, akitokea Cyprus alikokwenda baada ya kutimka Bongo.
Ndiku aliyemuoa Uwoya Julai, 2009, ameacha mke (Uwoya) na mwanaye Krish Bongo huku akisema staa wa huyo wa filamu za Kibongo atamkumbuka.

chanzo:GPL
No comments:
Post a Comment