Pichani kushoto ni aliyekuwa Mgeni rasmi kwenye usiku wa kumbu kumbu ya Marehemu Steven Kanumba,Meya wa Manispaa ya Kinondoni,Mh Yusuph Mwenda akipokea tuzo ya heshima kutoka kwa Mama wa Marehemu Steven Kanumba,kwa niaba ya Mh Rais Jakaya Kikwete,kwenye maadhimisho ya kumbukumbu ya kutimiza mwaka mmoja tangu kufarikii kwa nyota huyo wa Filamu hapa nchini na kwingineko.Kumbukumbu hizo zimefanyika jana jioni kwenye viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar na kuhudhuriwa na wasanii mbalimbali wa tasnia hiyo,wasanii wa muziki na kada nyinginezo mbalimbali,aidha katika Kumbukumbu hiyo pia kulizinduliwa Filamu ya mwisho aliyokuwa akiigiza Marehemu Kanumba kabla ya kufariki iliyoitwa Love & Power. |
No comments:
Post a Comment