Tuesday 21 May 2013

Rais Obama ajiandaa kwa ziara Afrika 21 Mei, 2013 - Saa 09:59 GMT Facebook Twitter Tuma kwa rafiki yako Chapisha Rais wa Marekani Barack Obama atazuru Afrika kwa mara ya tatu Rais wa Marekani Barack Obama anatarajiwa kuzuru Senegal, Afrika Kusini na Tanzania mwezi Juni. Hii ni kwa mujibu wa taarifa kutoka ikulu ya White house. Rais Obama atakutana na watunga sheria na wafanyabiashara pamoja na viongozi wa asasi za kijamii. Taarifa zinazohusiana Barack Obama Ziara ya Obama itaanza tarehe 26 Juni hadi 3 Julai na itakuwa ziara yake ya pili Kusini mwa jagwa la Sahara akiwa rais wa Marekani. Alizuru Ghana mwaka 2009 . Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton na mwenzake George W Bush, wote walizuru Afrika wakati wa muhula wao wa pili wa utawala. Clinton alizuru nchi sita wakati Bush akizuru nchi tano. ''Rais atatilia mkazo uhusiano kati ya Marekani na baadhi ya nchi za kiafrika ambazo zinakuwa ikiwemo maswala kama ukuwaji wa uchumi, uekezaji na biashara pamoja na kukuza taasisi za kidemokrasia na kuendelea kukuza viongozi wa kizazi kijacho Afrika,'' ilinukuu taarifa kutoka ikulu ya White House. Ziara ya Obama pia itatilia mkazo kukuza uhusiano kati ya Marekani na watu wa bara la Afrika ili kuendeleza ushirikiano wa kikanda, amani na ukuwaji. Wadadisi wanasema kuwa ziara kama hizi hufanywa sana na marais wa Marekani hasa baada ya kuondokewa na kazi ngumu ya kampeini za uchaguzi na shinikizo za ndani ya nchi. Wakati huohuo, tisho linaloongezeka kutoka kwa wapiganaji wa kiisilamu nchini Mali, limefanya kanda hiyo kumulikwa zaidi na Marekani. Bi Michel Obama ataambatana na mumewe katika ziara hiyo.



Rais wa Marekani Barack Obama atazuru Afrika kwa mara ya tatu

Rais wa Marekani Barack Obama anatarajiwa kuzuru Senegal, Afrika Kusini na Tanzania mwezi Juni. Hii ni kwa mujibu wa taarifa kutoka ikulu ya White house.
Rais Obama atakutana na watunga sheria na wafanyabiashara pamoja na viongozi wa asasi za kijamii.

Alizuru Ghana mwaka 2009 .Ziara ya Obama itaanza tarehe 26 Juni hadi 3 Julai na itakuwa ziara yake ya pili Kusini mwa jagwa la Sahara akiwa rais wa Marekani.
Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton na mwenzake George W Bush, wote walizuru Afrika wakati wa muhula wao wa pili wa utawala.
Clinton alizuru nchi sita wakati Bush akizuru nchi tano.
''Rais atatilia mkazo uhusiano kati ya Marekani na baadhi ya nchi za kiafrika ambazo zinakuwa ikiwemo maswala kama ukuwaji wa uchumi, uekezaji na biashara pamoja na kukuza taasisi za kidemokrasia na kuendelea kukuza viongozi wa kizazi kijacho Afrika,'' ilinukuu taarifa kutoka ikulu ya White House.
Ziara ya Obama pia itatilia mkazo kukuza uhusiano kati ya Marekani na watu wa bara la Afrika ili kuendeleza ushirikiano wa kikanda, amani na ukuwaji.
Wadadisi wanasema kuwa ziara kama hizi hufanywa sana na marais wa Marekani hasa baada ya kuondokewa na kazi ngumu ya kampeini za uchaguzi na shinikizo za ndani ya nchi.
Wakati huohuo, tisho linaloongezeka kutoka kwa wapiganaji wa kiisilamu nchini Mali, limefanya kanda hiyo kumulikwa zaidi na Marekani. Bi Michel Obama ataambatana na mumewe katika ziara hiyo.
bbcswahili

No comments:

Post a Comment