Wednesday, 3 November 2010

lunchtime leo"UGALI DAGAA NA TEMBELE"



Mahitaji


  • Dagaa wakavu (dry anchovies packet 1)
  • Unga wa ugali (corn meal flour 1/4 kilo)
  • Matembele ya kukaushwa (dried sweet potato leaves, handful)
  • Nyanya ya kopo (tin tomato 1)
  • Kitunguu maji (onion 2)
  • Limao (lemon 1/4)
  • Pilipili mbuzi nzima bila kukata (habanero chili 1, do not chop)
  • Chumvi (salt kiasi)
  • Mafuta (vegetable oil) 
  • Hoho (green pepper 1)
  • Kitunguu swaum (garlic 5 cloves)
  • Tangawizi (ginger 1 kijiko cha chai)
  • Binzari ya curry (Curry powder 1/2 kijiko cha chai)
Matayarisho
Safisha dagaa kwa kutoa vichwa na utumbo kisha waoshe na uwakaushe na kitchen towel na uwaweke pembeni. Baada ya hapo katakata, vitunguu na hoho kisha weka pembeni. Baada ya hapo weka sufuria jikoni na utie mafuta yakisha pata moto tia dagaa na uwakaange mpaka wawe wa brown, kisha tia kitunguu swaum,curry powder na tangawizi, kaanga kidogo kisha malizia kwa kutia vitunguu maji, hoho,pilipili,chumvi na ukamulie limao. Kaanga kwa muda wa dakika 3-4 na hakikisha vitunguu na hoho haviivi sana na hapo dagaa watakuwa tayari.

Baada ya hapo yaoshe na uyaloweka matembele (kama ni makavu) kwa muda wa dakika 15, Kisha yatoe na uyaweke kwenye sufuria pamoja na kitunguu, nyanya, chumvi ,kamulia limao kidogo, pilipili na maji kiasi. acha matembele yachemke kwa muda wa dakika 20 na uhakikishe yameiva kwa kuwa laini. Baada ya hapo yapike mpaka maji yote yakauke na mafuta yatok na hapo matembele yatakuwa tayari.

Ukisha maliza kupika dagaa na matembele andaa ugali.waswahili wengi najua mnaelewa jisi ya kusonga ugali.kwa mlio sverige tembele frozen lakini linapatikana taj mahal,dagaa msinunue ica maana zile za ica ni spesho kwa mbwa na paka,ila ukienda lile duka la wa-west pale hotorget chini utapata dagaa.

No comments:

Post a Comment