Friday, 5 November 2010

UKISTAAJABU YA MUSA!



PADR AMLAWITI MFANYAKAZI WA NDANI WA PAROKIA..
JESHI la polisi mkoani Kilimanjaro linamsaka Padri Stanslaus Sala wa parokia ya Mtakatifu Theresa Lego Muro,jimbo la Moshi katika kata ya Kilema Kusini kwa tuhuma ya kumlawiti mfanyakazi wa kiume wa parokia hiyo mwenye umri wa miaka 14 (Jina limehifadhiwa).

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanaro Lucas Ng’hobko aliithibitisha kupoea kwa taarifa hiyo na kwamba ameagiza padri huyo akamatwe.

“Nimepokea taarifa hiyo jana kutoka kwa wasaidizi wangu na tayari tunafanyia kazi ,anatafutwa kwanza huyu mtuhumiwa wakati upelelezi uiendelea ili kuthibitisha endapo ni kweli amefanya kitendo hicho na ikithibitika tutampelkea mahakamani”alisema Ng’hoboko.


Alisema taarifa za tukio hilo zilifikishwa kituoni Oktoba 31 mwaka huu kufungua jalada ambalo lilipewa namba MS/RB/14614/2010 na kupewa fomu namba 3 (PF 3) kwa ajili ya matibabu ya kijana huyo ambaye alitibiwa hospitali ya mkoa ya Mawenzi.


“Walifika kituoni kufungua jalada na kupatiwa PF 3 kwa ajili ya matibabu,lakini sisi bado hatujaiona inawezekana baada ya kupata matibabu wakaondoka nayo ,tumekwisha sikiliza upande mmoja lakini pia tunahitaji kusikia na upande wa pili”alisema Ng’hoboko.


Awali akizungumza na Tz daima jana mzazi wa kiume wa mtoto huyo,Amati Lyamuya aliyekuwa, ameambatana na wananchi zaidi ya 10 alisema tukio hilo lilitokea Oktoba 30 mwaka huu,majira ya saa 2 usiku.


Alisema taarifa za mtoto wake kufanyiwa kitendo hicho zilitolewa na mlinzi baada ya kijana huyo kuonekana kukereka na kitendo hicho kilichofanywa na kiongozi mkubwa kama huyo wa dini.

“Hatukuwa na taarifa yoyote juu ya taarifa ya vitendo vinavyofanywa na huyu Padri ,mlinzi wa parokia ambaye ni mmasai ndiye aliyenda kuwaeleza wazee wa kanisa ambao na wao walikuja kuwaeleza wanakijiji, tukaamua kuandamana”alisema Lyamuya.

Akisimulia tukio hilo ,kijana huyo alisema Padri huyo alimchukua baada ya kuhitimu darasa la saba kwa ajili ya kufanya kazi za kulisha mifugo kwenye Parokia hiyo huku akisubiri matokeo yake.

Alisema siku ya tukio,Padri alimuita mlinzi na kumwagiza akamuite kijana huyo kwenye chumba chake,ambapo baada ya kufika alieleza kuwa anastahili kupewa adhabu na kwamba ataenda kuadhibiwa eneo la mbali na parokia hiyo.

Bila kujua kosa lake kijana huyo alisema waliondoka na alimueleza kuwa wanakwenda eneo la Seminari ya Karumari lakini walipofika eneo la Kisanja ambako kuna msitu ,padri huyo alimtaka kijana huyo ashuke kwenye gari na kumfuata kwa upande wake ambapo alifunga mlango mmoja na kumuegemeza kwenye mlango wa
dereva.

“Baada ya kufika hapo msituni alisimamisha gari akaniambia nishuke na kwenda kwenye mlango wa upande wake ili anipe maelekezo kutoka kwa baba yangu,niliamini na kumfuata’alisema kijana huyo .

Nilipofika alinikandamiza kwenye mlango wa dereva na kunitoa kaptula na nguo ya ndani na kisha kuanza kunilawiti nilijaribi kujiokoa lakini sikufanikiwa ”aliongeza kijana huyo.

Alidai baada ya kumaliza alimwambia apande kwenye gari na kurudi parokiani ambako alienda moja kwa moja chumbani kwake huku akilia kwa uchungu kutokana na kitendo kile.

“Baaada ya kufika chumbani kwangu majira ya saa 5 na 6 Padri alirudi tena kugonga mlango lakini sikufungua’alisema kijana huyo.


Alidai kesho yake majira ya saa 2 asubuhi padri huyo alimfuata na kumpa mche mmoja wa sabuni na rozali na kumtaka asiseme popote jambo hilo huku akimuahidi zawadi nyingi zaidi.

Zaidi ya wananchi 10 wakiwa wameandamana na mtoto huyo walifika
kwenye kituo kikuu cha polisi mjini Moshi na kufungua jalada lenye
namba MS/RB/14614/2010 na kupewa fomu namba 3 (PF3) ya matibabu kwenye hospitali ya mkoa ya Mawenzi.

Kwa upande wake afisa Mtendaji wa kata,Adamu Mbuya,alisema aliletewa taarifa hizo wakati akiwa ofisini kwake na mwenyekiti wa kijiji,ambapo walimpeleka
hospitalini na kuonekana kuwa amelawitiwa na kujeruhiwa vibaya.

Alisema baada ya kuta taarifa kituo cha polisi walitakiwa kwenda kumkamata Padri huyo lakini zoezi hilo lilishindikana kutokana na polisi kuwa katika zoezi la uchaguzi ,ambapo polisi waliwaambia jalada la kesi hiyo limepelekwa kituo kidogo cha Himo.

Hata hivyo Mbuya alisema jana wakiwa na askari polisi wawili walienda kwenye parokia hiyo na mkuu wa kituo lakini hawakufanikiwa kumpata padri huyo

SOURCE:gpl

No comments:

Post a Comment