Tuesday, 27 September 2011

kwanini spidi ya ku-update blog inapungua??

wakuu wadau wakubwa wa hii blog,ni siku nyingi sasa spidi yetu ya blog ya isaackin kuweka matukio inaenda kwa kusua sua,hiyo yote inatokana na mabadiliko ya hali ya hewa na pia madhara ya kukatika kwa umeme wa mara kwa mara na pia hata ajali niliyopata nilipoteza vitendea kazi karibia vyote,kwani nilipata ajali niitokea kazini
hivyo basi mnaodhani blog ndio inaelekea ukingoni laah hasha blog ndio kwaaanza inapiga zoezi la push-ups na sarakasi ili tuje kuibuka kivingine tena tukipata mtandao sahihi.
hivi sasa wandugu tuvumiliane kwani tutaweka kile kinachopatikana na kufanya kinachowezekana kuwawekea matukio tunayojitahidi kupata.kama nilivyowajulisha mwanzo kwamba base ya blog ni burudani na starehe no steress no politiki.
hivyo msishangae kwamba matukio mengi yaliyopo humu ni burudani kwa kwenda mbere.jingine ni kwamba najitahidi kushughulika na blog kwa muda wangu wa ziada kwani shughuli nyingi ni za kutafuta mkate wa kila siku na nepi za milton.
hivyo nawaomba sana wadau wangu tuendelee kuwa pamoja kwa kipindi hiki kigumu cha mpito teh teh,tumefunga mikanda kwa petrol,tumefunga mikanda kwa umeme tumefunga mikanda kwa hali ngumu ya maisha sasa tujifunge mikanda pia kwa bulogu.kibongo bongo kila kitu politiki bandugu.
nina mikasa mingi ya kueleza na maphoto tupeane muda tu uhondo unakuja.

kwa herini umeme unabip apa nimalizie ukatike.

No comments:

Post a Comment