Thursday, 27 October 2011

RAIS KIKWETE AKUTANA NA WANAJUMUIA WANAOISHI NCHINI AUSTRALIA


 
Rais Jakaya Kikwete akizungumza na Mwenyekiti wa watanzania waishio Australia Asimwe Kabunga katika mkutano unaowajumuisha watanzania waishio Australia okt, 26-2011. Rais Jakaya Kikwete pamoja wanajumuia ya watanzania wanaoishi Australia wamezungumzia masuala mbalimbali ya maendeleo.
 
Baadhi ya wanajumuia wanaoishi nchini Australia wakimsikiliza. Rais Jakaya Kikwete hayupo pichani alipokutana nao Okt.26.2011 mjini Perth Australia.

 
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (kulia) akipokea maua kutoka kwa mweka Hazina wa Jumuia ya Watanzania waishio Australia Maryam Powell jana walipokutana na wanajumia mjini Perth Australia. Rais Jakaya Kikwete alikutana na wanajumuia kuzungumza mambo mbalimbali ya maendeleo na kijamii, Rais yupo nchini Australia kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa jumuia ya madola (Commonwealth Heads of Government Meeting- CHOGM 2011, utakaanza Oktoba 28-30, 2011.
 
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akibadilisha mawazo na mwanajumuia wa Australia Dr.Joseph Masika wakati Rais Jakaya Kikwete alipokutana na wanajumuia wanaoishi Australia 0ktoba 26, 2011 na kuzungumza nao mambo mbalimbali ya maendeleo ya nchi yetu.
 
Baadhi ya wanajumuia wanaoishi nchini Australia wakimsikiliza Rais Jakaya Kikwete hayupo pichani alipokutana nao Okt.26.2011 mjini Perth Australia.
 
Picha ya pamoja ya wanajumuia wa kike wanaoishi Australia pamoja na Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete baada ya kuamlizika mkutano wa Rais Kikwete na Watanzania wanaoishi Australia, jana.
 
Mama Salma Kikwete akisalimiana na mmoja wa wanajumuia.

Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO

No comments:

Post a Comment