Na Mwandishi Wetu
WAKATI shindano la kumsaka Miss Dar
Intercollege 2012 likitarajiwa kufanyika Juni 22 kwenye ukumbi wa Makumbusho ya
Taifa , uliopo mkabala na chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) duka la vipodozi la
Shear Illusions,pamoja na mbunifu maarufu wa mavazi,Mustafa Hassanali wamejitosa
kudhamini shindano hilo .
Awali shindano hilo
lilipangwa kufanyika juni 8 kabla ya kusogezwa mbele kutokana na sababu
mbalimbali ikiwemo baadhi ya warembo kuwa katika mitihani pamoja na mafunzo yao kwa vitendo ‘Field’.
Mratibu wa Shindano hilo Dina Ismail alimesema kwamba
Shear lenye matawi yake jengo la Millennium Tower na Mlimani City linajihusha
na uuzaji wa vipodozi halisi ‘original’ kutoka nje ya nchi litatoa vipodozi kwa
warembo watakaoshiriki,huku Hassanali atatoa zawadi ya magauni ya warembo.
Alisema maandalizi kwa ajili ya shindano hilo yanaendelea ambapo leo warembo hao ambao awali
walikuwa wakifanya mazoezi kwenye hoteli ya Lamada, jana walihamishia kambi yao kwenye hoteli ya
Grand Villa iliyopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Dina ameongeza kuwa mpaka sasa wameshapatikana
warembo 13 ambao wapo chini ya ukufunzi wa Marylidya Boniface, huku kwa upande
wa shoo wakinolewa na dansa aliyepata kufanya vema miaka ya nyuma, Bob Rich.
“Mwaka huu tumejipanga vema kuhakikisha mmoja ya
warembo kutoka Miss Dar Intercollege
anafanya vema katika fainali za Miss Tanzania ,”alisema Dina.
Warembo watakaoshiriki shindano hilo
wanatoka vyuo vya Biashara (CBE), Uandishi wa Habari (DSJ) na Time,
Ustawi wa Jamii, Usimamizi wa Fedha (IFM) na Chuo Kikuu huria (OUT
ambapo taji linashikiliwa na Rose Msuya kutoka IFM, huku mshindi wa pili wa
mwaka jana, Blessing Ngowi alitinga fainali za Miss Tanzania.
Dina aliwataja warembo hao kuwa ni pamoja na
Veronica Ngota, Rose Muchunguzi, Nancy Maganga, Hilda Edward, Diana
Nyakisinda, Neema Michael, Veronica Yollla, Jacquiline Cliff, Sharifa Ibrahim,
Natasha Deo, Saada Suleiman, Rose Masanja na Jamila Hassan.
Shindano hilo limedhaminiwa na kampuni ya Bia
Tanzania (TBL) kupitia bia ya Redd’s,Dodoma Wine, Ndege Insurance, Skylight
Band,Lamada Hotel, Screen Masters,Makumbusho ya Taifa, Mustafa Hassanali, Grand
Villa Hotel, Clouds Fm na blog za Michuzi, Mamapipiro, Bin Zubeiry,Mtaa kwa
Mtaa na Fullshangwe.
No comments:
Post a Comment