haruna boban
Wazungu wamrudisha Boban Dar es Salaam
UONGOZI wa klabu ya Syrianska ya Sweden umemrejesha nyumbani kiungo wa zamani wa Gefle IF, Haruna Moshi ili ajifue zaidi kabla ya kupewa nafasi nyingine ya kufanya majaribio akiwa fiti.
Kocha Mkuu wa Syrianska, Ozcan Melkemichel ameliambia Championi Jumatatu kwamba, wamekubaliana na Boban pamoja na wakala wake, Damas Ndumbaro kuwa kiungo huyo anapaswa kujifua zaidi ili arejee nchini humo mwezi ujao.
“Lazima tufanye hivyo, benchi la ufundi limeona ni mchezaji mzuri. Lakini hakuwa na mazoezi ya kutosha wakati anakuja huku. Tumezungumza naye na ametueleza hakuwa anashiriki mashindano yoyote kwa kutokuwa na timu.
“Kwetu si kitu kibaya kwa kuwa kiuwezo tumeona yuko safi, sasa tutakuwa na mechi za kirafiki kuanzia Januari katikati.
Sasa watu wote wanaenda kwenye sikukuu na tunaona hatakuwa na nafasi nzuri ya kujifua hapa sababu ya hali ya hewa. Tumemtaka arudi kipindi hicho ili aweze kumalizia nafasi hiyo ya pili ya majaribio halafu tutatoa jibu,” alisema Melkemichel.
Boban tayari amerejea nchini na kueleza ingekuwa vigumu kwake kujifua vya kutosha akiwa nchini humo kutokana na baridi kali inayotokana na barafu kumwagika hadi kuzuia viwanja kutumika.
Awali, Boban alikuwa akiichezea Gefle IF ya Sweden, lakini aliamua kuvunja mkataba na kurejea nyumbani kabla ya kurudi tena nchini humo kwa ajili ya kufanya majaribio.
Baadhi ya timu za Sweden pia zimekuwa zikionyesha nia ya kumsajili, moja wapo ni GAIS ingawa, hapo awali kumekuwa na taarifa kwamba Boban hakuvutiwa nayo.
source:GPL
ushauri kiduchu kwa bwana boban,kama kweli anahitaji kucheza soka la kulipwa,ajitahidi kupiga zoezi ili akirudi tena hapa akubalike asajiliwe.inabidi akaze buti kweli,maana yaelekea hata yule agent wake ana moyo kweli kwa mafanikio ya boban na ndio maana anamtafutia timu mara kwa mara ajaribu.boban inabidi pia aelewe kwamba mafanikio hayaji siku moja ni mtihani na mitihani mpaka hapo unapo succeed,hii biashara ya nenda rudi nenda rudi inazidi kumuharibia,na usikute hawa syrianska wamemtosa baada ya kupewa feed-back ya tabia yake aliyoifanya alipokuwa gävle if.inabidi boban aelewe kwamba kile alichokifanya kule wale jamaa(gävle if) wamerekodi,na hawataficha wala kudanganya kuiambia timu yeyote iliyopo hapa inayokuhitaji yale uliyoyafanya ulipokuwa nao.mabaya au mazuri.hapo ndio mwenyewe utakumbuka nini ulifanya kibaya au kizuri na ambacho kinaweza kukuponza katika utafutaji wako wote.nahisi kabisa yawezekana nafasi ya wewe kuchezea syrianska ilikuwepo wazi na jamaa wameweka longolongo baada ya kuulizia file lako kule kwenye ile timu uliyopakaza.yawezekana wale wameeleza mambo yako yote na ndio maana wanakutosa kwa vijisababu visivyoeleweka.anyway niwewe mwenyewe unajua kinachoendelea.kama ni kweli sababu niliyotoa ndiyo iliyosababisha,basi tena mzee utafute uelekeo wa kwenda cheza nchi nyingine yeyote ulaya,maana kama ikiwa ni sweden tena lazima mwisho watarejea kuuliza tabia yako kule kwa timu uliyotaja umechezea before(gävle) na wale wakiulizwa hawatachoka kumwaga utumbo wote uliofanya kule kama upo.ndio tunavyoishi hapa usishangae.mwisho hii ni tafakuri yangu tu,kama kweli issue ni mazoezi tu fanya kwa sana ukirudi tena uwaonyeshe kwamba wewe ni chaguo linalofaa.
nakutakia mafanikio mema katika kujenga maisha yako(sio taifa letu lililouzwa).
karibu tena sitoki-homu.
No comments:
Post a Comment