Saturday 25 August 2012

MAPISHI TOKA NYUMBANI:NYAMA YA KUSAGA


Haya mdau nina pishi dogo tu hapa napenda kulishare nawewe.Ni pishi la mboga ya nyama ya kusaga iliyoliwa na ugali pamoja na mboga ya majani ya mchicha.Hapa ntakuekea tu kuhusiana na mboga ya nyama ya kusaga.Ni mboga rahisi kuandaa na pia kuiva upesi.
Nikiwa napika huwa napenda kuandaaa kila kitu kiwe tayari ili nikianza nimeanza,mahitaji yetu kama unavyooona ni karoti,hoho na kitunguu maji.
Nilitwanga tangawizi mbichi nikaichanganya na nyama yangu ya kusaga.
Nikaweka frying pan jikoni na mafuta kidogo tu yalipopata moto tu kitunguu nikaweka na kukikaanga mpaka kikawa brown...
Nikatia nyama na kuikaanga
Halafu nikafunikia kwa dk 5 iive

Nikaweka limao na pilipili....
 Halafu nikaweka zile hoho na karoti,sijatumia nyanya ila ukipenda unaweza kuweka nyanya.
Nikafunikia kwa dk 5 tu...
Kama nilivyosema ni mboga ya haraka sana ndani ya kk 20 tu inakuwa imeiva.Kwangu ililiwa kwa ugali na mboga ya majani ya mchicha.Lakini inaweza kuliwa na wali,ugali,chapati,chips,ndizi za kukaanga au kuchoma,makaroni n.k

recipe na picha kwahisani ya dinamariosblog

No comments:

Post a Comment