Mwanamuziki
Kofii Olomide kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo akizungumza na
waandishi wa habari hawapo pichani leo kwenye hoteli ya serena Dar es
salaam, wakati alipozungumzia onesho lake linalotarajiwa kufanyika
katika viwanja vya Leaders kesho jumamosi, ikiwa ni kuadhimsha
shamrashamra za sikukuu kwa maonyesho kabambe yatakayofanyika Jijini Dar
es salaam, Mwanza kwenye uwanja wa CCM Kirumba, maonyesho hayo
yanadhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti kupitia bia yake ya Tusker
Lager yakipewa jina laTUSKER CARNIVALS CELEBRATIONS FEATURING KOFFI OLOMIDE!
Mwanamuziki huyo amesema ili kuwa
mwanamuziki mzuri Tanzania ni nchi nzuri na muhimu kwa wanamuziki katika
kujipima ili kujua kuwa ni mwanamuziki wa kiwango gani. Akaongeza kwa
kusema “Namshukuru Rafiki yangu mkubwa na Mkurugenzi wa kampuni ya
Clouds Media Group Bw. Joseph Kusaga kwa kunifanya niwe tajiri hivyo
naipenda sana Tanzania ni nchi Muhimu kwangu” akamaliza Kofii Olomide
Baada ya onesho la Leaders Kesho
mwanamuziki Kofii Olomide jumapili atafanya onesho lingine jijini
Mwanza, ambako wakazi wa Mwanza watapata burudani ya mwanamuziki huyo
Gwiji wa muziki Afrika
Mkurugenzi
mtendaji wa Kampuni ya bia ya Serengeti Bw. Steve Ganon akizungumza
katika mkutano huo na kukaribisha ujio wa maonyesho hayo ambayo yatawapa
burudani wananchi hasa kipindi hiki cha kuelekea sikukuu za Krismass.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Clouds Media Group Bw Joseph Kussaga akimkaribisha
mwanamuziki Kofii Olomide ili kuongea na waandishi wa habari kuhusu
maonyesho yake hayo yatakayofanyika jijini Dar es salaam na Mwanza.
Mkurugenzi
wa Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti Bw. Ephraim Mafuru
akizungumzia mipango na utaratibu mzima wa maonesho ya mwanamuziki Kofii
Olomide na jinsi kampuni hiyo ilivyojipanga kuwapa mashabiki Burudani
bora kabisa kupitia bia yake ya Tusker Lager.
Mkurugenzi
wa Mawasiliano na Uhusiano Kampuni ya bia ya Serengeti Bi. Nandi
Mwiyombela akimkaribisha mkurugenzi wa Masoko wa kampuni hiyo Bw Ephraim
Mafuru ili kuongea na wanahabari katika mkutano huo.
Mwanamuziki
Kofii Olomide akisalimiana na Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya bia ya
Serengeti Bw. Steve Gannon mara baada ya kuwasili katika chumba cha
mkutano leo, Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni hiyo Bw. Ephraim
Mafuru.
Mwanamuziki
Kofii Olomide akisalimiana na Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya bia
ya Serengeti Bw. Ephraim Mafuru mara baada ya kuwasili kwenye chumba cha
mkutano na waandishi wa habari leo, katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa
kampuni hiyo Bw. Steve Gannon.
Mwanamuziki
Kofii Olomide akisaini katika bango maalum linalowahimiza watu kuacha
kuendesha huku wakiwa wamelewa pombe katika kampeni ya kupunguza ajali
barabarani ya Kunywa Pombe Kistaarabu inayoendeshwa na kampuni hiyo kwa
wateja wake, anayeshuhudia tukio hilo kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa
kampuni ya bia ya Serengeti Bw. Steve Gannon.
kulia katika picha ni Anitha Msangi Meneja Msoko wa Tusker Lager,
Maurice Njowoka Meneja wa Kinywaji cha Tusker, Sialouise Shayo Brand
Executive na Agnes Kiondo kutoka Serengeti wakiwa katikia mkutano huo.
kulia ni Steve Gannon Mkurugenzi Mtendaji SBL, Ephraim Mfuru Mkurugenzi
wa Masoko SBL na Nandi Mwiyombela Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano
SBL wakimuangalia kwa makini mwanamuziki Kofii Olimide wakati akiongea
na wanahabari.
Mwanamuziki
Kofii Olomide akiwasili katika chumba cha mkutano uliofanyika kwenye
hoteli ya Serena Dar es salaam, kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya bia ya
Serengeti Bw. Steve Gannon na kushoto na Mkurugenzi wa Kampuni ya
Clouds Media Group Bw. Joseph Kusaga wakifuatana naye.
Chanzo:fullshangweblog
No comments:
Post a Comment