Friday, 18 June 2010

LOVENESS LOVE DIVA NA KISA CHAKE CHA MAPENZI



Mtangazaji wa Kipindi cha Ala za Roho wa Radio Clouds FM, Loveness Dominick Malinzi ‘Diva’ ameibuka na kusema kuwa, hana hamu na aliyekuwa mpenzi wake, Mohammed Hassan ‘Morack’ na wala hataki kumsikia.
Akiongea na Ijumaa hivi karibuni Diva alisema kuwa, ni kweli alikuwa amezama kwenye dimbwi la mapenzi na msanii huyo kiasi cha kufikia hatua ya kumfanyia mambo makubwa lakini anashangaa kuambulia shukrani ya mateke.

“Mimi na Morack kweli tulikuwa wapenzi tukaachana baada ya kushindwana na kila mtu akachukua time yake, cha ajabu baada ya kutemana amekuwa akinifanyia mambo ya ajabu sana.

“Yeye ndiye aliyenitongoza nami nikadhani ni mwanaume sahihi nikamkubali nikijua maisha yatakwenda freshi lakini kila siku ilikuwa na maudhi ya aina yake mpaka nikajuta,” alisema Diva na kuongeza:

“Naomba niseme tu kwamba, kwasasa simhitaji tena Morack, ninaye Sean wangu ambaye yuko Marekani, nampenda na tuna mpango wa kuoana,hivyo wanaomtaka Morack wamchukue tu mimi hanifai nami simfai,” alisema Diva.
Gazeti hili lilijitahidi kumtafuta Morack ili azungumzie madai hayo bila mafanikio jitihada hizo zinaendelea
source:global publishers

pole sana mama,ushauri wangu mimi huo ni mwanzo tu jikaze endeleza maisha tu,visa vya mapenzi viko viiingi na safari yako bado ndefu sana,kila la kheri na mupenzi wako mupya.

2 comments:

  1. Mbona mnapindisha mambo jamani? jalibuni kuwa wakweli kuhusu mpendwa wetu DIVA. Unajua haiwezekani DIVA apatikane alafu Morack hasipatikane. tunaitaji mambo yote yawekwe wazi. kwani hatupendi DIVA aptikane na matatizo hayo ambayo bado kwa watu tunasikia minong'ono kuwa Bado DIVA anaendelea na Kijana huyo. Jalibu kumtafuta morack na mambo yaende safi.

    Ba de way. we don need our cmmrade to be involved in such scandl like dis.

    2 our star DIVA Everthing shld be opened!

    Magege. email: sonatmagege@gmail.com

    Tanx!

    ReplyDelete
  2. Diva is a slut...

    ReplyDelete