Thursday, 23 September 2010

WASANII WANAPOKUMBUKANA WAKATI WA SHIDA


MZEE KIPARA
 kwa sasa mze anasumbuliwa na matatizo ya miguu na mengineyo

kanumba alipomtembelea mzee kipara
kanumba akijitolea mchango wake kidogo kumuwezesha mzee siku mbili tatu.

najua wengi mnamfahamu  mzee kipara,kwani licha ya kuwa waanzilishi wa kwanza kabisa wa kundi la kaole pia mtakuwa mnamkumbuka enzi hizo alipokuwa akiigiza na mzee jangala,mama haambiliki na tomato miaka hiyoo,mi nilikuwa mmojawapo kati ya mashabiki wa kubwa wa hiyo michezo ya kuigiza enzi hizo.ulikuwa hunikosi sebuleni pembeni ya RTD saa tatu na nusu ukiwasikiliza hawa wazee wakiwajibika kisanii. kutufurahisha.hata kipindi cha pwagu na pwaguzi pia walikuwa wakifurahisha sana.sasa kama mnavyojua tena hali ya maisha ya nchi yetu ilivyo,licha ya umahiri wote huo wa huyu mzee lakini haujaweza kumsaidia chochote cha maana kwa kipindi chote cha muda wote aliokuwa akihangaika huku na kule katika kuikuza sanaa ya mtanzania,mpaka sasa mzee anasumbuliwa na matatizo kama hayo.ya miguu.ni matatizo madogo sana lakini kwake ni makubwa kwani hana sapoti yeyote zaidi ya kujihangaikia mwenyewe,utashangaa kwamba baada ya kutumika sana huyu mzee kaachwa kama hivi!anyway nisiseme sana huyu mzee anahitaji msaada na kama una moyo kumsaidia wasiliana na kanumba kwenye blog yake kanumbathegreat.blogspot.com/  huko kuna mawasiliano yote na yeye atawasilisha msaada wako kwa mzee kipara.

No comments:

Post a Comment