Vipimo
Mchele wa basmati 3 Vikombe*Dengu 2 vikombe
Viazi 3 vikubwa
Kitunguu 2 kubwa
Nyanya 2 Pilipili mbichi kubwa 3 Pilipilimanga ½ kijiko cha chai.
Garama Masala (bizari mchanganyiko) 1 kijiko cha chai
Supu ya vidonge (stock cubes) 2 vidonge
Chumvi kiasi, Mafuta ¼ kikombe
Zaafarani 1 kijiko cha chai
Samaki wa kuchoma
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
* Dengu kama sio za tayari kwenye kopo, roweka na zichemshe hadi ziwive
Masala Ya Dengu:1. Zaafarani – iroweke katika maji ya vugu-vugu (warm) ya chini ya robo kikombe weka kando.
2. Osha mchele, roweka.
3. Menya viazi na vitunguu, katakata vitunguu, na nyanya , weka kando.
4. Katakata viazi vipande vidogo vidogo kwa umbo la mchemraba (cubes).
5. Katika sufuria tia mafuta yakipata moto, tia viazi ukaange kidogo kwa moto mdogo mdogo hadi kukaribia kuwiva, toa weka kando.
6. Kaanga vitunguu hadi vigeuka rangi ya hudhurungi isiyokoza (light brown) kisha tia nyanya ukaange kidogo. 7. Tia vidonge vya supu (stock cubes) uvivuruge katika mchanganyiko, katakata pilipili mbichi kwa urefu tia, uendelee kukakaanga. Tia bizari, chumvi.
8. Zima moto, changanya dengu na viazi katika mchanganyiko huo.
Wali:
1. Chemsha mchele kama kawaida ya kupika wali mweupe, kiini kiwe kimewiva nusu yake.
2. Chuja maji kisha changanya katika mchanganyiko wa dengu. 3. Nyunyizia zaafarani, uchanganye wali na mchanganyiko kidogo tu.
4. Funika acha uive katika mtoto mdogo mdogo au tia katika oveni hadi uive kama kawaida ya kupika wali. 5. Pakua katika sahani na tolea na samaki yoyote wa kuchoma.
piga menyu hiyo kisha pumzika kwa muda kabla hujaenda kufakamia norlan guld ama slotts guld vinginevyo utarudisha change kwa wenyewe.
No comments:
Post a Comment