Saturday 17 September 2011

MTANZANIA MBARONI CANADA KWA KESI YA UBAKAJI



Na Mwandishi Wetu
MTANZANIA Steven Konyaki (30),  mkazi wa Palestina- Sinza, Dar es Salaam ambaye kwa sasa anaishi Marekani, amedakwa na serikali ya Canada akituhumiwa kwa ubakaji wa wanawake watatu, akiwemo binti wa miaka 14 nchini Marekani, mitandao imejulisha.
Konyaki (pichani)  kwa nyakati tofauti anadaiwa kuwabaka  wanawake hao na kukimbilia nchini humo kwa lengo la kujificha.

Habari zinadai kwamba, baada ya kutenda kosa kwa mara ya pili, mtuhumiwa huyo alikimbilia nchini Canada ambapo Agosti 8, mwaka huu alidakwa na polisi akiwa kwenye mji mkuu wa nchi hiyo, Toronto.
Idara ya uhamiaji nchini humo inafanya taratibu za kumrudisha mtuhumiwa Marekani ili akasomewe mashitaka ya mara pili, kumbaka mwanamke mzee na binti huyo Hii ni mara ya pili kwa Mbongo huyo kutuhumiwa kutenda kosa hilo ambapo Novemba 4, 2010 akiwa kwenye makazi yake Hamley jijini Lynn, Massachusetts, Marekani alitenda kosa kama hilo kwa bibi kizee mmoja (62) kati ya wawili waliomlalamikia. Alifikishwa kwenye mahakama ya Wilaya ya Lynn.    
'
Katika mashtaka ya kwanza, mtuhumiwa huyo akijitetea mbele ya polisi, alisema siku ya tukio alikuwa amelewa hivyo hakujua alichokuwa akikifanya na kwamba wakati akimwingilia bibi kizee huyo alijua ni msichana.

Katika kesi hiyo, mtuhumiwa aliachiwa huru kwa dhamana ya dola za Kimarekani 1,500 (zinakaribia shilingi milioni tatu za Kibongo) huku kesi yake ikiendelea kufanyiwa upelelezi wa kina.

Baada ya taarifa hizi, mwandishi wetu alimtafuta kaka wa mtuhumiwa anayeishi Sinza, Dar ambaye alisema hawana habari hizo.

“Hatuna taarifa kama amefikishwa tena mahakamani na hata hiyo habari ya kwanza hatuna taarifa,” alisema kaka '
huyo anayejulikana kwa jina la Paul  Konyaki.
chanzo:GPL

1 comment: