Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundega akiongea na waandishi wa habari leo kwenye Hoteli ya JB Belmonte jijini Dar es salaam wakati alipotangaza udhamini wa Miss Tanzania 2012 ambapo Redds imedhamini mashindano hayo mwaka huu kwa milioni 700, katika picha kutoka kulia ni Miss Tanzania Salha Israel, Vick Kimaro Meneja wa Redds na Meneja Masoko wa TBL Fimbo Butala.
Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundega na Meneja Masoko wa TBL Fimbo Butala. wakijiandaa kukabidhiana hati mara baada ya kusaini mkataba wa udhamini wa mashindano ya Redds Miss Tanzania, wanaoshuhudia ni Mwenyekiti wa kamati ya Miss Tanzania Prashant Patel kushoto nyuma na Vick Kimaro Meneja wa kinywaji cha Redds.
Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundega na Meneja Masoko wa TBL Fimbo Butala. wakikabidhiana hati mara baada ya kusaini mkataba wa udhamini wa mashindano ya Redds Miss Tanzania, wanaoshuhudia ni Mwenyekiti wa kamati ya Miss Tanzania Prashant Patel kushoto nyuma na Vick Kimaro Meneja wa kinywaji cha Redds.
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd’s Original leo imetangaza rasmi kuchukua nafasi ya “Mdhamini Mkuu” wa shindano kubwa kabisa la urembo hapa nchini lijulikanalo kama “Miss Tanzania”.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, meneja masoko wa TBL Bw. Fimbo Butallah alisema; Redds Original, leo inatangaza kuwa ndio wadhamini wakuu wa mashindano ya urembo Tanzania, yanayojulikana kama “Miss Tanzania”. Kwa udhamini huu, mashindano haya sasa yatajulikana kama “REDDS MISS TANZANIA 2012”. Kwa miaka kadhaa sasa Redds Original imekuwa ikishiriki katika mashindano haya kama mdhamini mwenza, yaani “Kinywaji rasmi cha Miss Tanzania”. Hivyo leo tunapiga hatua nyingine kubwa katika historia ya tasnia hii ya urembo hapa nchini kwa kuwa mdhamini mkuu wa mashindano ya Miss Tanzania.
Katika kuonesha kuwa Redds Original, imedhamiria kwa dhati kuendeleza tasnia hii, leo tumesaini mkataba wa udhamini wa mashindano haya kwa kipindi cha miaka mitatu, yaani 2012 hadi 2014. Hii inawahakikishia wapenzi na mashabiki wa mashindano haya kuwa wataendelea kushuhudia mashindano haya na kuburudika na kinywaji cha Redds Original kwa kipindi chote hiki. Alisema Butallah.
Nae Meneja wa Kinywaji cha Redds Original Bi. Victoria Kimaro alisisitiza juu ya udhamini wa mashindano haya kuanzia ngazi za chini hadi ngazi ya Taifa. Udhamini huu mkubwa wa mashindano ya Miss Tanzania unajumuisha udhamini tutakaotoa katika maeneo mbali mbali kwa ngazi za vitongoji hadi Taifa. Tunawaahidi mashabiki wote wa mashindano haya na wadau wa tasnia ya urembo kujiandaa kwa burudani ya hali ya juu.
Akizungumzia udhamini huo, Mkurugenzi wa LINO Agency waandaaji wa shindano la Miss Tanzania, Bw. Hasim Lundenga alisema; Kwa niaba ya kamati ya Miss Tanzania napenda kutoa shukurani za dhati kwa TBL kupitia kinywaji chake cha Redds Original kwa udhamini huu, na tunatangaza rasmi kuwa mashindano haya sasa yataitwa “Redds Miss Tanzania’. Kitu kikubwa tunachowashukuru wadhamini wetu ni mkataba ambao tumesaini hii leo, ukituhakikishia udhamini wa mashindano haya kwa miaka mitatu.
Kwa mara nyingine tunawapongeza zaidi Redds original kwa kuwa mstari wa mbele katika kuendeleza tasnia hii ya urembo hapa nchini. Tumekuwa nao bega kwa bega kwa miaka kadhaa sasa, na haiwezekani ukazungumzia tasnia ya urembo hapa nchini bila kuitaja Redds Original. Alisema Lundenga.
No comments:
Post a Comment