hapa ndio kituoni (mjini)ukitoka kijijini wanapaita K.K.K. ama kyimo kijiji kitulifu main road ya kwenda malawi kupitia tukuyu.and yes its a jesus factory
soma ujumbe hapo mbele
of course hii ni njia ya kuendea kijijini kwetu kabisa asili ya mzee kinaitwa iponjola,kukutana na roli zimesheheni mizigo ya namna hii kawaida sana
barabara yao huko main road ni full mkeka toka kabla hatujapata uhuru ndio maana ni ngumu kwenda kuwaongopea kipindi cha kampeni kwamba utajenga bara bara.
wakenya nao hawajabaki nyuma ,niliona hii picha wametangaza mahali kwamba iko tukuyu kenya
chai fresh kabisa ikiwa bado shamba,kule jamaa hawanunui majani ya chai dukani wala sukari,majani wanachuma live fresh toka shamba kisha wanaanika na kupondaponda tayari kwa chai,sukari pia miwa inapondwa pondwa mpaka inalainika kisha inaanikwa na ikikauka kabisa inatwangwa kwenye kinu unapata sukari safi tu,kipindi hiyo nikimtembelea babu alisisitiza tuende na maandazi tu kayamiss kila kitu kipo.
vichochoro vya huko ni vimezibwa na migomba huku na huko,so huwezi toka jasho maana njia nzima ni full kivuli
ukiwa huko huna haja ya kubeba mwamvuli,mvua ikianza unakata jani la mgomba unajifunika huyooo safari na muziki,pia usisahau jani hilo la mgomba linaweza kutengeneza kijiko safi ukalia makande au ubwabwa bila tabu.
KARIBUNI TUKUYU JAMENI,MI NIPO HUKU NALIMA MAHINDI
No comments:
Post a Comment