Meli ya Azam Marine inayoitwa Azam SeaLink 1 ikiwasili katika bandari ya Visiwani Zanzibar kwa mara kwanza.
Baadhi ya wakazi wa Zanzibar wakipiga picha Meli hiyo iliyowasili Visiwani Zanzibar leo.
Mzee Said Salim Bakheresa (mwenye nguo nyeusi) akikagua mazingira ya Meli hiyo baada ya kuwasili Bandari ya Zanzibar leo.
Sehemu ya Parking yenye uwezo wa kuingiza magari 200.
Muonekano wa ndani wa Lounge ya kumpzikia wasafiri.
Muonekano wa nje. (Picha na Omar Said wa Kampuni ya Bakheresa).
Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi Zanzibar
Kampuni
ya Azam Marine inayomiliki boti ziendazo kasi hapa nchini, leo
imeingiza meli mpya na ya kisasa itakayochukua zaiidi ya abiria 1500 na
magari 200.
Meneja
Mkuu wa Kampuni ya Azam Marine, Bw. Hussein Mohammed Saidi, amesema leo
mjini Zanzibar kuwa meli hiyo ambayo itafanya safari zake kati ya Dar
es Salaam, zanzibar na Pemba itatoza nauli nafuu kwa abiria wake.
Amesema meli hiyo ambayo inatarajiwa kuanza safari zake mara baada ya kukamilisha taratibu za mamlaka mbalimbali.
Meli hiyo inayoitwa AZAM SEALINKI ni ya kisasa katika ukanda huu wa Mwambao wa nchi za Kusini na Pembe ya Afrika.
Bw.
Hussein amesema Meli hiyo ambayo imetengenezwa nchini Ugiriki na
inatayarishiwa eneo maalumu litakalotumika kwa kupakia na kushusha
abiria na mizigo yakiwemo magari.
Amesema
meli hiyo itasafiri kwa muda wa saa tatu kutoka Dar es salaam na
Zanzibar na saa 4 kutoka Zanzibar na Pemba ama saa 7 kutoka dar es
salaam na Pemba.
Amesema
pamoja na kuwasili kwa Meli hiyo, Kampuni ya Azam pia inatarajia kuleta
meli nyingine ya abiiria inayojulikana kama Kilimanjaro namba 4.
Kwa
upande wao, baadhi ya wananchi wa Visiwa vya zanzibar wamepongeza ujio
wa meli hiyo lakini wakaitaka serikali kuendelea kudhibiti uingizwaji wa
meli chakavu na kukuu ili kuepuka uwezekano wa kutokea ajali za mara
kwa mara.
Bwana
Rajabu Khamisi mkazi wa Pemba na Bi. Rehema Omari wa mjini Zanzibar,
wamesema kuna haja ya Serikali kusimamia ukomo wa nauli ili kila
mwananchi aweze kusafiri kutoka sehemu moja na nyingine kwani wamesema
vipato havilingani.
No comments:
Post a Comment