Wednesday, 2 March 2011

MRISHO NGASSA AFUMANIWA



WAKATI timu yake ya  Azam leo ikisaka nafasi ya kurudi kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom katika mchezo dhidi ya Majimaji, mshambuliaji wake mahiri Mrisho Ngassa amekumbwa na kashfa ya kimapenzi.

Ngassa anadaiwa kukutwa akiwa na mwanadada mwingine nje ya ndoa yake, kisha kunusurika kupigwa na mama mzazi wa mkewe (mkwe).

Tukio hilo ambalo lilivuta umati wa watu linadaiwa lilitokea Yombo Dovya, Manispaa ya Temeke na baadaye mkasa huo kuhamia Mtoni Sabasaba, nyuma ya viwanja vya maonyesho, Sabasaba anapoishi mwanasoka huyo kinara wa mabao.

Akisimulia  mkasa huo kwa Mwananchi, mke wa mchezaji huyo, Latifa Mrisho Ngassa alisema kwa simu, ì Kama wewe  ni mwandishi wa habari, kimbia njoo hapa Sabasaba   na ikibidi chukua hata pikipiki ili uwahi, uje na kamera umtoe huyu jamaa kwani nimemfumania na ameamua kujifungia ndani."

Hata hivyo, baada ya dadika 30 mwanadada huyo akapiga tena simu  akisema kwamba mjumbe wa nyumba kumi alikuwa tayari ameshafika katika eneo la tukio kwa ajili ya kuwasuluhisha.

ìHuyu jamaa yangu amezidi kunidhalilisha kwani hata majirani wameshamchoka kwa tabia yake hii ( si vyema kuitaja gazetini),îaliongeza mke wa mchezaji huyo.

Ndipo Mwananchi ilipoamua kumtafuta mke wa mshambuliaji huyo kwa ajili ya kufahamu undani wa suala hilo, ndipo alipoeleza, ìHuyu ni mme wangu wa ndoa tena ndoa iliyofungwa kihalali kabisa, lakini kwa kipindi kirefu sasa amekuwa akinisumbua kwa tabia zake.î

ìKweli mimi nimechoka na tabia zake kiasi kwamba siwezi kuendelea kuvumilia ujinga wake huu kama ndio imeshindikana siwezi kulazimisha ndoa ni bora niondoke nirudi kwetu nikafiche aibu hii.

Alisema baada ya kupata taarifa kutoka kwa majirani kule Dovya alimchukua mama na mjomba wake, kisha wakaenda  eneo la tukio, lakini walipofika mumewe akajifungia ndani na kukataa kutoka.

ìKwa sasa mimi ninakaa kwetu  Tabata, lakini kila wakati majirani wamekuwa wakiniambia juu ya tabia zake za kukutwa na wanawake na wakati mwingine anaondoka nao kwenda kustarehe huku mimi akiniacha,îalidai mke huyo wa mwanasoka.

Alipoulizwa juu ya hatma ya ndoa yake, alisema ni mapema mno kuzungumzia hilo kwa sababu liko kwenye ngazi ya familia yao, hivyo ni vyema asubiri kwanza mpaka familia itakapokaa na kulizungumzia.

 Lakini, Mwananchi ilipofika katika eneo la  tukio saa 12:30 jioni na kukuta wahusika wameshatawanyika  baadhi ya majirani pamoja na mjumbe wa nyumba kumi walithibitisha kuwapo kwa tukio hilo.

ìNi kweli mama mkwe alikuja juu na kupiga mlango huku akimtaka mkwe (Ngassa) atoke na kutoa talaka ili aondoke na  binti yake kwani amechoshwa na tabia hizo chafu na za  kudhalilishwa anazofanyiwa binti yake na kudai kwamba kila anapouliza binti yake anaishia kupigwa,î alieleza mmoja wa majirani.

Mwananchi   ilimtafuta mama mkwe huyo, Octavia Kangati ambaye alisema: ìNi kweli tulifika nyumbani kwa mkwe wangu ili kufahamu undani wa tukio hilo, lakini sikuthubutu kujaribu kumpiga.î

ìMimi ni mama siwezi kuthubutu kumpiga mkwe wangu, bali hayo ni maneno  ya mitaani wala mjomba wake hakumpiga, bali katika kusuluhisha tofauti zao kukatokea kupishana kwa maneno,îaliongeza mama huyo.

Hata hivyo, alipoulizwa chanzo cha tukio hilo alikataa kulizungumzia kwa madai kuwa alikuwa safarini kuelekea Kibaya, Kiteto mkoani Manyara  ila akamtaka mwandishi wa Mwananchi amtafute siku nyingine.

Kwa upande wake, Ngassa alipoulizwa  kuhusu tukio hilo alijibu, ìNi kweli nilikuwa na dada mmoja ambaye alihitaji kupanga nyumba katika nyumba yangu na alipoletwa kwangu na madalali nikamchukua hadi kwenye nyumba iliyopo Yombo Dovya, ghafla nikaona kundi la watu akiwemo mke wangu pamoja na mama yake.î

ìKaka, haya mambo ni magumu,  tena yana lengo la kuniharibia, kunidhalilishana, mimi siwezi kufanya hivyo kwa sababu mke wangu nampenda, kwanza habari hizi mmezipata wapi, kwa sababu ni saa mbili tu tangu yalipotokea,"  alisema Ngassa.

Hata hivyo, alipotakiwa kueleza ukweli juu ya kunusurika kupigwa na mkwewe, mchezaji huyo alishindwa kulizungumzia na kumtaka mwandishi arudi siku nyingine ili apate ufafanuzi.

ìSiwezi kuzungumzia suala hilo kwa sasa nakuomba uniache kwanza kwa sababu kichwa changu kina mambo mengi, tafuta siku nyingine, lakini sio leo,îalisema Ngassa na kuingia kwenye gari na kuondoka katika eneo hilo.

Baba mzazi wa mchezaji, Khalfan Ngassa huyo alipotafutwa na Mwananchi  alisema kwa simu, ìNimepokea taarifa za tukio hilo, ni masikitiko sana kwa sababu hayo mambo yana lengo la kumharibia mwanangu maisha yake ya soka.î

ìSifahamu lolote kuhusu suala hilo, lakini nitawatafuta wanangu wote niongee nao  kwani nisipofanya hivyo nitachangia kumharibia mtoto wangu maisha yake hasa katika kipindi hiki cha kuisaidia timu yake kupata ubingwa wa Ligi ya Vodacom,îalisema Mzee Ngassa.

CHANZO:MWANANCHI

No comments:

Post a Comment