Tuesday, 8 March 2011

President's son from an oil-rich poor country orders $400 million luxury yacht

Teodoro Nguema Obiang Mangue
Taint of Corruption Is No Barrier to U.S. Visa - NYTimes.com



teodoro+obiang+nguema+malibu+mansion.jpg
Teodorin Nguema Obiang ...


kwa habari zaidi gonga HAPA

uliwahi kujiuliza kwanini bara la afrika watu ni maskini sana licha ya kuwa ndio bara linaloongoza kwa utajiri duniani??hata mimi sijui kwanini
maana hata rais wangu aliwahi kuulizwa baada ya kutafakari kwa muda akajibu hata yeye haelewi ni kwanini!

je ni kweli hatujui ni kwanini tunakuwa maskini??tunajua ila hatujui kama tunajua.

huyu bwana mkubwa hapo mtoto wa rais wa equatorial guinea na waziri wa kilimo mr
Teodoro Nguema Obiang Mangue ametoa oda  ya kutengenezewa luxury yacht yenye thamani ya dola 400 million.
!ndiyo dola 400 million bwana.na usidhani kakurupuka tu na kutaka kuoda hiyo boti hapana,jamaa ni maarufu kwa matumizi ya dizaini hiyo,anamiliki pia villa huko malibu lenye thamani ya dola 34million kama unavyoona picha pale juu,na private jet pia magari ya thamani ya kila dizaini unayojua wewe,na mwisho ni kwamba anammiliki pia yule rapper maarufu wa kike queen eve(inasemekana ndie anamchanganya sasa anahamishia pesa zote U.S).

bwana mkubwa huyu amekiri kwamba anapenda kuishi vizuri ndiyo,cha kushangaza sasa ni kwamba mshahara wake yeye kama waziri kwa mwezi hauzidi dola 7000/=,sasa ndio utajiuliza na kupata jibu mwenyewe hiyo ziada inatoka wapi??

haya tunayaongelea hapa sio matani,yapo na yanatokea katika karibia kila nchi afrika,rasilimali za nchi nzima badala ya kutumiwa kwa manufaa ya wananchi,zinaenda kutumiwa na mtu mmoja.

viongozi wamekuwa wabinafsi,hata Tanzania tunaona yanatokea haya,wakati wabunge wanajiidhinishia kuchukua mikopo ya mil 90 na kuchukua ma vx V8,hapo hapo wanaidhinisha serikali kununua bajaj zitumike kama ambulance,hao ndio viongozi waliochaguliwa na wananchi ili wawatumikie!
sasa hivi mbunge ama waziri akishalewa ukamsumbua kukutolea raia bastola na kutishia kuua ama kuua kabisa imekuwa kawaida,si tumeona juzi hapa muzee wa vijisenti kawagonga wale wadada wawili na wamefariki na yupo tu anadunda mitaani,ni nani anaweza sema ilikua ajali??
na ndio muzee wa visenti kakutwa na makosa ya kusababisha ajali na vifo na kuendesha gari isiyo na bima(akiwa bwii) lakini kaishia kupigwa faini ya sumni laki saba!
hiyo ndio bongo dale salama,sasa ukitaka kujua sheria inafanyaje kazi wewe kapuku jaribu tu hata kubishana na kiongozi ama hata familia yake cha moto utakiona.
ni wangapi mpaka sasa wako jela kisa tu wameonekana ama wanajifanya kujua zaidi ya viongozi hao.
haya yote yanafanyika na tunayaona,lakini nani mwenye sauti ya kupiga kelele ama kuuliza??kama hujipendi waweza fanya hivyo.
lakini ni lini watu watajikomboa kwenye mabavu haya yaliowazunguka miaka nenda rudi?hatujui.
katoka nyerere na kawawa wakaja watoto wa kawawa na nyerere,kapokea mwinyi sasa tuna mwinyi waziri pia .akaja makamba na sasa kuna kina february  makamba na nduguze,amekuja kikwete sasa kuna ridhwani anatrot kuja kupokea kijiti,kuna lowassa kuna mwanae lowassa yupo anatawala mahala,kuna nnauye sr aliyeondoka sasa kuna nnauye mkuu wa wilaya,kuna kingunge na wanae vingunge wengine na wengineo wengi yaani cheni ni hiyo hiyo ya chama twawala inatuzunguka tu.sielewi ina maana hamna watu wengine wenye uwezo wa kutawala zaidi ya hao?.
kesho itakuwa wajukuu wao,keshokutwa itakuwa vitukuu na vilembwe vyao humo humo serikalini,kwenye mabenki na taasisi zote za ulaji.
raia na wananchi wa kawaida mutaishia kuhongwa pilau na soda na tishet kipindi cha kampeni na uchaguzi basi,na kwa njaa inavyokaba munauza utu wenu kwa mgao miaka mitano+mitano(kidogo kidogo imefika miaka 50 sasa),sijui nani alaumiwe lakini hakuna
tuilaumu njaa,na wajanja viongozi wanajua kama raia wana njaa hivyo wana-twist tu kipindi njaa inapoletwa  ije katika spidi gani.mpaka mnalainika tu.

inabidi tuamke wananchi

2 comments:

  1. yani Isac hapa ndo unaponikosha na manewz km haya ni udaku ila wa ukweli tena unachoma sn hasa ukiwa mwafrika kudadeki. Asa lakini Isac jamani hili swala la move unalichukuliaje mbn tunageukana bana? move 1 wikend 1 yani pati 1 ijumaa ingine Jpili au mosi tukukoshe basi na ilo juamani watu wako

    ReplyDelete
  2. mzazi una maneno makali sana,taratibu tutafika huko walipofika wenzentu,nakupa saluti mzazi.Wewe ni moja ya watu muhimu sana ktk ile dunia yetu ya tatu.Mdau tumba

    ReplyDelete